Nenda kwa yaliyomo

Mtaguso wa Konstanz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mtaguso wa Kostansa)

Mtaguso wa Konstanz (1414-1418) unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa 16.

Mtaguso huu uliitishwa na antipapa Yohane XXIII kwa ombi la kaisari Sigismund wa Ujerumani ukathibitishwa na Papa Gregori XII (1406-1415).

Ulifanyika Konstanz (Ujerumani).

Lengo kuu lilikuwa kumaliza Farakano la Kanisa la Magharibi lililofikia hatua ya kuona maaskofu watatu kujidai Papa kwa wakati mmoja.

Malengo mengine yalikuwa kung’oa uzushi na kurekebisha Kanisa “katika kichwa na viungo vyake”.

Hatimaye Papa Gregori XII alikubali kujiuzulu, wapinzani wake wawili waliondolewa, na Papa Martin V akachaguliwa.

Ulikuwa mtaguso muhimu kwa wingi wa waliohudhuria (makardinali 29, maaskofu 186, maabati zaidi ya 100 na wataalamu 300 hivi), muda (vikao 55) na mafanikio, ingawa majaribio yake ya mapinduzi yalishindikana, hasa ulipodai kuwa na mamlaka ya juu kuliko Papa.

Kati ya maamuzi mengine kuna hukumu dhidi ya John Wyclif na Jan Hus kama wazushi.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtaguso wa Konstanz kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.