Canterbury

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
mji wa Canterbury pembezon mwa mto stour
bendera ya Canterbury



Canterbury
Canterbury is located in Uingereza
Canterbury
Canterbury

Mahali pa mji wa Canterbury katika Uingereza

Majiranukta: 51°16′30″N 1°5′13″E / 51.27500°N 1.08694°E / 51.27500; 1.08694
Nchi Uingereza
Mkoa South East
Wilaya Kent
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 43,432
Tovuti:  www.canterbury.co.uk

Canterbury ni mji wa mkoa wa Kent, kusini mwa Uingereza, si mbali na London. Una wakazi 42.259 (2001).

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ulianza kukaliwa karne nyingi K.K. na kuitwa Cantuaria. Baada ya kuvamiwa na Warumi chini ya Julius Kaisari mwaka 55 K.K. ulifanywa Forum commerciale (yaani mahali pa biashara).

Kuanzia mwaka 560 ukawa mji mkuu wa ufalme wa Kijerumani wa Kent, na mwaka 597 Augustino wa Canterbury akitokea Roma akaanzisha huko dayosisi ya kwanza ya Kilatini katika kisiwa cha Britania. Kwa ubatizo wa mfalme, uinjilishaji ulipiga hatua kubwa.

Tangu hapo, mji huo ukawa na umuhimu hasa upande wa Ukristo, kwa sababu dayosisi hiyo ilizaa taratibu nyingine zote za kisiwa hicho.

Kwa msingi huo, Askofu mkuu wa Canterbury akawa mkuu wa Maaskofu wote wa Uingereza, halafu wa Waanglikana wote duniani.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Uingereza bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Canterbury kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.