Dola la Papa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya dola mnamo mwaka 1700, lilipofikia kuwa na eneo kubwa zaidi, katikati ya Italia, mbali ya miji ya Benevento na Pontecorvo Italia kusini na wilaya ya Venaissin na mji wa Avignon Ufaransa kusini.

Dola la Papa lilikuwa nchi huru chini ya himaya ya Papa kuanzia miaka ya 700 hadi 1870.

Chanzo chake ni uvamizi wa makabila ya Wagermanik uliobomoa Dola la Roma upande wa magharibi wa Bahari ya Kati. Wenyeji, wengi wao wakiwa Wakristo Wakatoliki, walimkimbilia Papa kama kiongozi wao atakayeweza kuwasaidia katika matatizo.

Baadaye Wafaranki walikubali kumuachia Papa mamlaka ya kisiasa juu ya maeneo mbalimbali nje ya Roma. Polepole maeneo yaliongezwa hata kufikia mikoa 3 na nusu ya Italia ya leo: Lazio, Umbria, Marche na sehemu ya Emilia-Romagna.

Dola lilikoma tarehe 20 Septemba 1870, jeshi la Italia lilipoteka mkoa na mji wa Roma, isipokuwa mtaa wa Vatikano.

Kwa mapatano ya tarehe 11 Februari 1929, badala yake ilianzishwa Mji wa Vatikani, nchi ndogo kuliko zote duniani (kilometa mraba 0.44, wakazi 600 hivi), lakini huru ili mamlaka ya kiroho ya Papa isiingiliwe na watawala wa dunia kama ilivyotokea zamani.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dola la Papa kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.