Nenda kwa yaliyomo

Tassili n'Ajjer

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya hifadhi ya Tassili N'ajjer

Tassili n'Ajjer ni safu ya milima katika Jangwa la Sahara nchini Aljeria. Kutokana na mimea iliyoweza kudumu hapa imetambuliwa kama hifadhi ya bioanwai. Kuna pia michoro mingi ya miambani kutoka enzi ya historia ya awali. Eneo lote limekuwa hifadhi ya kitaifa na kupokewa na UNESCO katika orodha ya urithi wa dunia.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Tassili n'Ajjer inaenea kwa kilomita za mraba 72,000 kwenye mpaka wa Aljeria na Libya na Niger. Inapakana na milima ya Ahaggar. Ndani yake kuna mlima wa Adrar Afao unaofikia mita 2,158 juu ya UB. Mji ulio karibu ni Djanet.

Bioanwai[hariri | hariri chanzo]

Bonde kwenye Tassili N'ajjer lenye miti.

Kimo cha nyanda za juu kinapunguza joto kiasi kulingana na tambarare za jangwa katika mazingira yake. Miamba inaweza kutunza maji ndani yake na hivyo kuwezesha uoto zaidi kuliko jangwani. Kwa hiyo mabonde ya juu huwa na uoto wa miti iliyopotea tayari penginepo kama Cupressus dupreziana na Myrtus nivellei. Michoro ya miambani inaonyesha kwamba zamani milima ilijaa wanyamapori wa aina nyingi lakini mamba walipotea tangu miaka 100. Kondoo mwitu bado wanapatikana.

Sanaa ya mwambani[hariri | hariri chanzo]

Mwanaakiolojia Mfaransa Lhote mbele ya mwamba unaooyesha picha za watu waliopanda farasi

Milima hii inajulikana sana kwa sanaa ya miambani, ambayo ni hasa oicha elfu kadhaa zilizochongwa kwenye uso wa mwamba na kuonyesha watu, ngoma zao na wanyama kama vile ng'ombe, tembo, twiga na kiboko. Picha hizi zimekadiriwa kuwa na umri wa miaka elfu kadhaa, za kale zina miaka 12,000[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Tassili N'Ajjer, Algeria, tovuti ya africanworldheritagesites.org, iliangaliwa Novemba 2019

Kujisomea[hariri | hariri chanzo]

 • Bahn, Paul G. (1998) The Cambridge Illustrated History of Prehistoric Art Cambridge, Cambridge University Press.
 • Bradley, R (2000) An archaeology of natural places London, Routledge.
 • Bruce-Lockhart, J and Wright, J (2000) Difficult and Dangerous Roads: Hugh Clapperton's Travels in the Sahara and Fezzan 1822-1825
 • Chippindale, Chris and Tacon, S-C (eds) (1998) The Archaeology of Rock Art Cambridge, Cambridge University Press.
 • Clottes, J. (2002): World Rock Art. Los Angeles: Getty Publications.
 • Coulson, D and Campbell, Alec (2001) African Rock Art: Paintings and Engravings on Stone New York, Harry N Abrams.
 • Frison-Roche, Roger (1965) Carnets Sahariens Paris, Flammarion
 • Holl, Augustin F.C. (2004) Saharan Rock Art, Archaeology of Tassilian Pastoralist Icongraphy
 • Lajoux, Jean-Dominique (1977) Tassili n'Ajjer: Art Rupestre du Sahara Préhistorique Paris, Le Chêne.
 • Lajoux, Jean-Dominique (1962), Merveilles du Tassili n'Ajjer (The rock paintings of Tassili in translation), Le Chêne, Paris.
 • Le Quellec, J-L (1998) Art Rupestre et Prehistoire du Sahara. Le Messak Libyen Paris: Editions Payot et Rivages, Bibliothèque Scientifique Payot.
 • Lhote, Henri (1959, reprinted 1973) The Search for the Tassili Frescoes: The story of the prehistoric rock-paintings of the Sahara London.
 • Lhote, Henri (1958, 1973, 1992, 2006) À la découverte des fresques du Tassili, Arthaud, Paris.
 • Mattingly, D (ed) (forthcoming) The archaeology of the Fezzan.
 • Muzzolini, A (1997) "Saharan Rock Art", in Vogel, J O (ed) Encyclopedia of Precolonial Africa Walnut Creek: 347-353.
 • Van Albada, A. and Van Albada, A.-M. (2000): La Montagne des Hommes-Chiens: Art Rupestre du Messak Lybien Paris, Seuil.
 • Whitley, D S (ed) (2001) Handbook of Rock Art Research New York: Altamira Press.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Tassili n'Ajjer Cultural Park travel guide kutoka Wikisafiri