Kairuan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kairouan

Kairuan ( Kiarabu ), pia Kairouan au Al Qayrawān ni mji mkuu wa Wilaya ya Kairuan nchini Tunisia. Mji umepokewa na UNESCO katika orodha ya Urithi wa Dunia.

Mji ulianzishwa na Waumawiya baada ya upanuzi wa Waarabu Waislamu mnamo mwaka 670. [1] Katika kipindi cha Khalifa Mu'awiya (661-680) kilikuwa kituo muhimu cha usomi wa Kiislamu wa Kisunni na ujifunzaji wa Qur'ani [2] na hivyo kuvutia Waislamu wengi kutoka sehemu mbali mbali za ulimwengu. Hadhi yake ilipitwa tu na Makka na Madina na Yerusalemu . Msikiti mtakatifu wa Uqba uko katika mji huo. [3]

Mnamo 2014, jiji lilikuwa na wakazi wapatao 187,000.

Mskiti Kuu ya Kairouan

Picha za Kairuan[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Nagendra Kr Singh, International encyclopaedia of Islamic dynasties. Anmol Publications PVT. LTD. 2002. page 1006
  2. (2004) The New Cambridge Medieval History, Volume 2; Volume 4. Cambridge University Press, 696. ISBN 9780521414111. 
  3. (1996) Hutchinson Encyclopedia 1996 Edition. Helicon Publishing Ltd, Oxford, 572. ISBN 1-85986-107-5. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]