Majira ya saa
Majira ya saa ni maeneo la dunia yenye umbo la mlia unaoenea kati ya ncha zote mbili yaani kuanzia kaskazini hadi kusini. Ndani ya mlia huu muda sanifu ni uleule, yaani masaa huonyesha saa ileile.
Saa zetu zinalenga kulingana na mwendo wa jua angani. Wakati wa jua kufika kwenye kilele chake angani kabisa ni katikati ya mchana au ni saa 6 mchana.
Kwenye ikweta saa ya upweo ni saa 12 asubuhi. Mahali pote panapopatikana kwenye mstari mmoja kati ya kaskazini na kusini huwa pamoja kimuda wakati wa mchana. Lakini maeneo ambayo ni mbali zaidi upande wa mashariki au magharibi huwa na wakati tofauti maana kwao jua lina upweo au mchana wakati tofauti ama mapema au baadaye.
Zamani kila mji au kijiji kiliweza kuamulia wakati wake kulingana na jua. Tangu kupatikana kwa njia za mawasiliano ya haraka kama simu, barua pepe au usafiri kwa kutumia reli, gari au eropleni imekuwa muhimu kuwa na saa za kulingana kati ya mahali mbalimbali. Hii ni msingi wa kuanzisha kanda wakati. Kwa hiyo kati ya Dar es Salaam na Mbeya hali halisi kuna tofauti ya zaidi ya nusu zaa. Maanake tukipiga simu wakati wa kucha kutoka Dar kwa mtu huko Mbeya kwake jua bado liko angani maanake yuko magharibi na huko jua linazama baadaye. Lakini ndani ya nchi ya Tanzania miji yote imepangwa kanda wakati moja hivyo kote ni saa ileile.