Abdelmadjid Tebboune

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Abdelmadjid Tebboune

Abdelmadjid Tebboune
Nchi Algeria
Kazi yake Rais teule wa Algeria
Abdelmadjid Tebboune
عبد المجيد تبون

Taking office
Succeeding Abdelkader Bensalah (kaimu)

Waziri Mkuu wa Algeria
Rais Abdelaziz Bouteflika
mtangulizi Abdelmalek Sellal
aliyemfuata Ahmed Ouyahia

tarehe ya kuzaliwa 17 Novemba 1945 (1945-11-17) (umri 78)
Mécheria, Algeria
chama urais aligombea bila chama

Abdelmadjid Tebboune (kwa Kiarabu: عبد المجيد تبون; alizaliwa Mécheria, Algeria, 17 Novemba 1945) ni mwanasiasa wa Algeria aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo kuanzia Mei 2017 hadi Agosti 2017. Kwenye Desemba 2019 alichaguliwa kuwa rais wa nchi. Hapo awali alikuwa Waziri wa Nyumba kutoka 2001 hadi 2002 na tena kutoka 2012 hadi 2017.

Tebboune alihitimu kutoka Chuo cha Kitaifa cha Utawala mnamo 1965. [1]

Tebboune alikuwa Waziri-Mjumbe wa Serikali za Mitaa kuanzia 1991 hadi 1992. Baadaye, chini ya Rais Abdelaziz Bouteflika, alihudumu serikalini kama Waziri wa Mawasiliano na Utamaduni kutoka 1999 hadi 2000 na kisha kama waziri msaidizi wa Serikali ya Mitaa kuanzia 2000 hadi 2001. Alikuwa Waziri wa Nyumba na Mipango wa Miji kutoka 2001 hadi 2002. Miaka kumi baadaye, mnamo 2012, alirudi katika wadhifa wa Waziri wa Nyumba katika serikali ya Waziri Mkuu Abdelmalek Sellal . [2]

Kufuatia uchaguzi wa bunge wa Mei 2017, Rais Bouteflika alimteua Tebboune kuwa Waziri Mkuu tarehe 24 Mei 2017 lakini aliendelea kwa miezi mitatu pekee. Bouteflika alimfukuza kazi na kumteua Ahmed Ouyahia tarehe 15 Agosti 2017; [3] Ouyahia alichukua madaraka siku iliyofuata. [4]

Mnamo Desemba 12, 2019, kufuatia uchaguzi wa rais wa Algeria, Tebboune alichaguliwa kuwa rais, baada ya kupata asilimia 58 za kura. [5]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. من هو رئيس الحكومة الجزائرية عبد المجيد تبون؟ (Arabic). Al Jazeera.
  2. "Premier ministre d'Abdelaziz Bouteflika ?", 2017-05-25. Retrieved on November 2, 2019. (fr) Archived from the original on November 2, 2019. 
  3. Lamine Chikhi (15 August 2017). Algeria recalls veteran crisis manager Ouyahia as Prime Minister. Reuters. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-12-12. Iliwekwa mnamo 2019-12-14.
  4. Le Premier Ministre prend ses fonctions (French). Official website of the Prime Minister of Algeria (16 August 2017).
  5. Algeria election: Ex-PM to replace Bouteflika after boycotted poll. BBC (13 December 2019).