Nenda kwa yaliyomo

Andrea Avellino

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu yake huko Milano.

Andrea Avellino (Castronuovo di Sant'Andrea, Potenza, 1521Napoli, 10 Novemba 1608), alikuwa padri wa Italia[1] wakati wa Urekebisho wa Kikatoliki akajiunga[2] na aina mpya ya utawa aliyoianzisha Gaetano wa Thiene, maarufu kwa jina la Wateatini, akaieneza zaidi pamoja na kufanya utume.

Pamoja na kung'aa kwa maisha matakatifu na juhudi kwa wokovu wa wengine, alijifunga kwa nadhiri ngumu ya kupiga hatua kila siku kuelekea ukamilifu wa Kikristo, na hatimaye, akiwa mwingi wa stahili, alifariki altareni.[3].

Alitangazwa na Papa Urban VIII kuwa mwenye heri tarehe 14 Oktoba 1624, halafu Papa Klementi XI alimtangaza mtakatifu tarehe 22 Mei 1712.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[4].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Marejeo ya Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 411-412
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 360-361

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.