Jangwa la Chalbi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Jangwa la Chalbi ni jangwa dogo katika kaskazini ya Kenya kusini ya mpaka wa Ethiopia. Jangwa liko mashariki mwa Ziwa Turkana ambalo ni ziwa kubwa duniani linalodumu ndani ya jangwa. Mji wa North Horr umo katika jangwa hili. Mji mkubwa wa karibu ni Marsabit.

Jina la Chalbi limetoka katika lugha ya Wagabbra likimaananisha 'tupu'. Ni eneo lenye joto kubwa na yabisi katika Kenya.

Wenyeji naoishi kando lake na kuivuka ni Warendille na Wagabbra wanaotumia ngamia kwa usafiri. Umbo la jangwa hili ni tambarare kabisa. Inaaminiwa ya kwamba mika 10,000 ilikuwa ziwa kubwa. Dalili zake ni visukuku vya kijiwe vya samaki na konokono vinavyopatikana hapa.

Wakati wa mvua sehemu za jangwa zafunikwa tena na maji kama ziwa lisilo na kina kikubwa lakini hli hii haidumu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]