Miraa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Miraa
Catha edulis
Catha edulis
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae
(bila tabaka): Angiosperms
(bila tabaka): Eudicots
(bila tabaka): Rosids
Oda: Celastrales
Familia: Celastraceae
Jenasi: Catha
Spishi: C. edulis
(Vahl) Forssk. ex Endl.
Miraa ikiuzwa sokoni huko Somaliland
Vicha vya miraa

Miraa ni majani na vitawi ya mrungi, mti ulio na asili ya Pembe ya Afrika na Rasi ya Uarabuni inayojulikana pia kwa jina lake la Kiarabu Khat (قات, Catha edulis). Majani changa ya miraa hutafuniwa na kutumika kama kichochezi cha mwili na akili. Shirika la Afya Duniani (WHO) limeiweka miraa kwenye kundi la madawa ya kulevya.

Miraa hukua kama kichaka au mti mdogo kwa urefu wa mita 1-5 na wakati mwingine huweza kufika urefu wa mita 10 penye tabianchi ya ikweta. Kwa kawaida mimea inakua katika mazingira yenye ukame, kwa kiwango cha joto la 5-35 ° C (41-95 ° F). Majani yake ni ya kijani, yenye urefu wa sentimeta 5-10 (inchi 2-4) na upana wa sentimeta 1-4 (inchi 0.39-1.6).

Miraa huthibitiwa kwenye nchi mbalimbali kama vile Kanada, Ujerumani, Uingereza, na Marekani wakati biashara na matumizi yake ni halali kwenye nchi za Jibuti, Kenya, Uganda, Ethiopia, Somalia na Yemeni.

Miraa hujulikana kwa majina mbalimbali kama vile qat na gat huko Yemeni, qaat na jaad nchini Somalia, na chat huko Ethiopia. Pia inajulikana kama jimaa kwa Kioromo, mairungu kwa Kikikuyu na mayirungi kwa Kiganda. Miraa imekuwa ikitumiwa kwa karne nyingi katika Pembe ya Afrika na Peninsula ya Uarabuni. Huko, kutafuna miraa kulianza zamani hata kabla ya matumizi ya kahawa. Huko Uganda miraa hulimwa katika kanda ya Kati na baadhi ya maeneo ya kanda ya Magharibi ya nchi. Nchini Kenya hulimwa katika eneo la Meru.

Ingawa tabia ya kutafuna miraa iko zaidi katika nchi ilipotokea, mmea huu hulimwa pia katika nchi za Afrika Kusini, Msumbiji, na Eswatini.

Majani mabichi hutafunwa na wakati mwingine hukaushwa na kutumiwa kama chai. Majani au sehemu nyembamba ya tawi huweza kutafunwa kwa karanga za kukanga au gamu ili iwe rahisi kutafuna. Katika nchi nyingi ambako miraa inatumika, mara nyingi watumiaji wake ni wanaume. Moja ya madhara yake ni kupoteza hamu ya chakula.

Miraa ni maarufu sana Yemeni ambapo kilimo chake hutumia rasilimali nyingi za kilimo. Inakadiriwa kuwa asilimia 40 ya maji ya nchi huelekea kumwagilia miraa na uzalishaji unaongezeka kwa asilimia 10 hadi 15 kila mwaka. Sababu moja kubwa ya kulimwa kwa miraa Yemeni ni mapato yanayotokana na zao hili. Nchini Kenya miraa huzalisha hasa katika eneo la Meru kwa ajili ya soko ya Somalia.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Chem template.svg Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Miraa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.