Nenda kwa yaliyomo

Eastleigh (Nairobi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Eastleigh, Nairobi)
Soko la Garissa, Eastleigh.

Eastleigh ni mtaa wa Nairobi nchini Kenya. Iko upande wa mashariki wa Naírobi mjini. Uwanja wa ndege wa kijeshi wa Eastleigh uko upande wa kaskazini ya mtaa. Mtaa wa mabanda wa Mathare Valley imepakana moja kwa moja na Eastleigh.

Eastleigh ni mtaa wa pekee nje ya Nairobi mjini (kitovu cha kibiashara) wenye mpangilio kwa namna ya jiji. Barabara zake zimepangwa kama miraba; First, Second na Third Avenue huenda sambabamba na barabara ndogo zinazokata kwa pembemraba zahesabiwa pia kama mtaa wa kwanza, wa pili, wa tatu, wa nne (First Street, Second Street n.k.). Nyumba nyingi ni za magorofa zinazofuatana bila nafasi ya bustani. Hii ni tofauti na eneo kubwa la Nairobi penye mabustani.

Mpangilio mzuri wa Eastleigh umerudi nyuma kwa sababu manisipaa ya Nairobi haikuangalia mtaa huu kwa muda mrefu. Kwa miaka mingi First Avenue pekee ilitunzwa lakini barabara za kando ziliharibika kabisa. Second Avenue imetengenezwa upya tangu mwaka 2006.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Eastleigh ilipangwa wakati wa ukoloni kama eneo la Wahíndi. Baada ya uhuru Wahindi wengi waliondoka au kuhama. Badala yao Wasomalia na Waethiopia wengi waliingia Eastleigh.

Kiutawala Eastleigh ni sehemu ya tarafa ya Pumwani ndani ya mkoa wa Nairobi.

Kati ya watu mashuhuri wa Eastleigh alikuwako Mohamed Amin aliyejulikaa kama mwanahabari na mpiga picha.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]