Nenda kwa yaliyomo

Chuo Kikuu cha Ufundi cha Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chuo Kikuu cha Ufundi cha Kenya (TU-K) ni chuo kikuu cha umma huko Nairobi, Kenya. Kiliandikishwa mnamo Januari 2013 na aliyekua rais wa wakati huo wa Kenya Mwai Kibaki.

historia

[hariri | hariri chanzo]

Chuo Kikuu cha Ufundi cha Kenya kilikua kutoka kwa Polytechnic ya Kenya. Kenya Polytechnic ilianzishwa mnamo mwaka 1961. [1] Mapendekezo ya kuanzishwa kwa taasisi ya ufundi jijini Nairobi yalitangazwa katika Ripoti ya Willoughby iliyochapishwa mnamo mwaka 1949. Hii ilisababisha kuundwa kwa Chuo cha Ufundi cha Royal cha Afrika Mashariki (RTCEA). [2]

Lengo lilikuwa kuanzisha chuo cha ufundi jijini Nairobi ambacho kitatoa elimu na mafunzo ya ufundi na viwango vya nusu taaluma kwa maeneo matatu ya Afrika Mashariki ambayo ni Kenya, Uganda, na Tanganyika. Ilikuwa muhimu wakati huo katika kila wilaya kuwe na wanafunzi walio kidhi vigezo vya kutosha kujiunga na RTCEA.Wakati Uganda na Tanganyika zilianzisha taasisi za kiufundi huko Kampala na Dar es Salaam kwaajili ya kuandaa watahiniwa kujiunga na RTCEA, Kenya iliamua kuanzisha mitiririko ya darasa chini ya jina la Taasisi ya Ufundi ya Kenya (KTI) huko RTCEA. [3] [4]

Kufikia mwaka 1960 ilikuwa imeamuliwa kwamba Chuo cha Ufundi cha Royal cha Afrika Mashariki kinapaswa kuongeza jukumu lake la kutoa digrii. Kwa hivyo mnamo 1960, RTCEA ilipewa mamlaka ya kutoa shahada za Chuo Kikuu cha London chini ya mpango maalum. kwaajili ya sifa hii mpya, chuo kilibadilishwa jina na kuitwa Royal College Nairobi[5]

  1. tukict (2013-01-31). "TU-K Profile - The Historical Background". The Technical University of Kenya (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-06-19. Iliwekwa mnamo 2021-06-20.
  2. tukict (2013-01-28). "The First Technical University in Kenya". The Technical University of Kenya (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-06-24. Iliwekwa mnamo 2021-06-20.
  3. tukict (2013-01-28). "The First Technical University in Kenya". The Technical University of Kenya (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-06-24. Iliwekwa mnamo 2021-06-20.
  4. tukict (2013-01-31). "TU-K Profile - The Historical Background". The Technical University of Kenya (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-06-19. Iliwekwa mnamo 2021-06-20.
  5. "From Royal Technical College to University of Nairobi | Taylor & Francis Group". Taylor & Francis (kwa Kiingereza). doi:10.4324/9781315134611-8. Iliwekwa mnamo 2021-06-20.
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Ufundi cha Kenya kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.