Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta
Jomo Kenyatta International Airport Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta | |||
---|---|---|---|
Faili:Kenya Airports Authority logo.png | |||
IATA: NBO – ICAO: HKJK | |||
Muhtasari | |||
Aina | Joint (Civil and Military) | ||
Opareta | Kenya Airports Authority | ||
Mahali | Nairobi, Kenya | ||
Kitovu cha | Fly540 Kenya Airways | ||
Mwinuko Juu ya UB |
5,327 ft / 1,624 m | ||
Anwani ya kijiografia | 01°19′09″S 036°55′39″E / 1.31917°S 36.92750°E | ||
Tovuti | |||
Njia ya kutua na kuruka ndege | |||
Mwelekeo | Urefu | Aina ya barabara | |
ft | m | ||
06/24 | 13,507 | 4,117 | Asphalt |
Takwimu (2016) | |||
abiria | 7,039,175 |
Uwanja wa ndege Kimataifa wa Jomo Kenyatta, uliofahamika kwanza kama uwanja wa ndege wa Embakasi na uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Nairobi, ndio uwanja unaopata wasafiri wengi sana katika Afrika ya Mashariki. Huu ni uwanja wa saba ulio na shughuli nyingi zaidi katika Afrika yote. Uwanja huu wa ndege ulipewa jina la Waziri Mkuu na Rais wa kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta.
Uwanja huu uko katika kitongoji cha Embakasi ulioko kusini-mashariki mwa Nairobi, kilomita 15 kutoka katikati mwa jiji la Nairobi. Barabara kuu ya Mombasa ipitiayo kando ya uwanja huu ndio barabara ya pekee kutoka Nairobi hadi ndani ya uwanja huu.
Kenya Airways na Fly540 huendesha shughuli zao ndani ya uwanja huu wa ndege kwa sababu ndicho kitovu cha shughuli nyingi muhimu.
Uwanja huu unatumia Ujia wa 06/24. Ujia wa 06 umewekwa vyombo na vifaa vya ILS, na hutumiwa nyakati za kupaa na kutua kwa ndege. Uwanja huu unahudumiwa na jumba moja lililojengwa miaka ya sabini. Kitovu chk “Embakasi”, kilichojengwa kabla ya 1960, kinatumika kama nyumba ya virago na pahala pa mafunzo kwa wanafunzi katika kikosi cha wanajeshi wa hewa .
Uwanja wa ndege ulihudumia abiria 7,039,175 katika mwaka wa 2016.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Uwanja wa ndege wa Nairobi ulifunguliwa mwezi Mei mwaka wa 1958, na Gavana wa mwisho wa Kenya, Everlyn Baring. Uwanja huu ulipaswa kufunguliwa na Malkia Elizabeth, Malkia Mama, lakini alichelewa kule Australia na hangeweza kuhudhuria sherehe hiyo.[1]
Baadaye mpisho unaotumika hivi sasa ulijengwa upande wa pili wa ujia wa ndege na uwanja ulibadilishwa jina na kuitwa Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Mpisho ule wa awali mara kwa mara huitwa uwanja wa Zamani wa Embakasi na hutumiwa na kikosi cha Kenya cha wanajeshi wa hewa.
Mpisho
[hariri | hariri chanzo]Mpisho wa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta una sehemu tatu ambazo hutumiwa kwa wanaowasili na wanaoondoka. Sehemu ya kwanza na ya pili hutumiwa mno mno kwa usafiri wa ng'ambo na sehemu ya tatu hutumiwa kwa usafiri wa humu nchini.
Wanaoondoka hujiwasilisha katika sehemu ya kwanza ama ya pili kulingana na wanakokwenda. Sehemu zote mbili zina pahali pa kujisajilisha ambapo panatumiwa teknolojia ya kisasa iitwayo CUTE (Common Use Terminal Equipment), na pahali ambapo watu hujaza stakabadhi za uhamisho, kabla ya kuelekea mahali pa kusubiri, kuondoka kwenye ghorofa ya kwanza. Kuna malango manane ya kuondoka yanayotumiwa kuabiri ndege. Wanaowasili hutumia malango yaya haya ili kuelekea mahala pa kujaza stakabadhi za uhamisho na baadaye huelekea jumba la kuwekea shehena katika ghorofa la chini kabisa. Jumba hili la shehena limeundwa kitaaluma kulingana na teknolojia za kisasa.
Kuna huduma za benki, magari ya kukodisha, wanaotembeza watalii na huduma za hoteli pale pa kuwasili. Katika sehemu ya kwanza na pili kuna vituo vya matwana ambapo matwana haya husafirisha wasafiri kuelekea mjini na kutoka mjini.
Hoteli ya Simba iko katika ghorofa la tano katika jumba maalum ambapo shughuli zote hutendeka. Kuna: hoteli iendeshwayo chini ya mwavuli wa Home Park katika sehemu ya kwanza, hoteli nyingine na mahali pa kujiburudisha na vileo katika sehemu ya pili, duka ndogo la vitu vya kula katika sehemu ya tatu na ukumbi mkubwa wa wasafiri wa kimataifa-zote zikiwa zimesimamiwa na NAS. Mashine za kuuza vinywaji vimewekwa katika kila sehemu.
Madawati ya usaidizi wa wasafiri yamewekwa katika kila sehemu na katika ukumbi wa wanaowasili na yamesimamiwa na ofisi ya Huduma kwa Wateja. Flight Information display systems (FIDS) na signage husaidia abiria kupata njia zao uwanjani mwa ndege.
Mipango ya upanuzi kwa miaka ijayo
[hariri | hariri chanzo]Tarehe 14 Oktoba 2005, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege vya Kenya (Kenya Airports Authority) ilitangaza mipango kabambe ya kupanua uwanja huu wa kimataifa wa Jomo Kenyatta. Kamati hii ilitangaza kuwa katika kipindi cha miaka miwili ijayo, viwanja vya ndege vitaweza kuboreshwa kote nchini, hasa mjini Nairobi. Mradi wa upanuzi ulichangiwa na ongezeko la abiria lilipotimu abiria milioni 4 ilhali uwanja huo ulijengewa abiria milioni 2.5.
Upanuzi huu wa uwanja wa ndege utazidisha zaidi ya maradufu ukubwa wake, kuanzia eneo la kuegeza ndege, ambalo kwa sasa halina nafasi ya kutosha, litapanuliwa na barabara za magari ya kukodisha zitajengwa. Sehemu za kupokea abiria wanaowasili na wanaoondoka zitatenganishwa kikamilifu, na eneo la kusubiri litakarabatiwa.
Upanuzi huu wa uwanja wa ndege utazidisha uwezo wa kustahimili abiria milioni 9 kwa mwaka. Gharama ya mradi huu ni dola milioni 100. Benki ya Dunia itatoa dola milioni 10. Awamu ya kwanza ya upanuzi ulianzia tarehe 29 Septemba 2006. Kwa sasa serikali bado inajadili ikiwa uwanja huu wa Jomo Kenyatta unapaswa kujengewa ujia wa ndege wa pili. Mjadala huu uliibuka wakati tukio lililofanya kufungwa kwa ujia unaotumiwa kwa siku moja
Kampuni za Ndege na Maeneo ya Usafiri
[hariri | hariri chanzo]Makampuni ya ndege | Vifiko |
---|---|
African Express Airways | Aden, Al Mukalla, Berbera, Dubai, Juba, Mogadishu, Mombasa, Sharjah |
Air Arabia | Sharjah |
Air India | Mumbai [ends 20 Januari] |
Air Italy | Milan-Malpensa, Rome-Fiumicino |
Air Madagascar | Antananarivo |
Air Mauritius | Mauritius |
Air Uganda | Entebbe |
Air Zimbabwe | Harare |
British Airways | London-Heathrow |
Brussels Airlines | Brussels |
Daallo Airlines | Djibouti, Hargeisa, Mogadishu |
East African Safari Air | Juba, Kisumu, Lokichogio |
EgyptAir | Cairo |
Emirates | Dubai |
Ethiopian Airlines | Addis Ababa |
Fly540 | Mombasa, Kisumu, Eldoret, Kitale, Lodwar, Lamu, Malindi, The Mara, Kilimanjaro, Entebbe, Zanzibar |
JetLink Express | Eldoret, Goma, Juba, Kisumu, Mombasa |
KLM | Amsterdam |
Kenya Airways | Abidjan, Accra, Addis Ababa, Amsterdam, Antananarivo, Bamako, Bangkok-Suvarnabhumi, Bujumbura, Cairo, Dar es Salaam, Dakar, Djibouti, Douala, Dubai, Entebbe, Freetown, Gaborone, Guangzhou, Harare, Hong Kong, Johannesburg, Khartoum, Kigali, Kinshasa, Kisumu, Lamu, Lagos, Lilongwe, London-Heathrow, Lubumbashi, Lusaka, Maputo, Mayotte, Mombasa, Monrovia, Moroni, Mumbai, Ndola, Paris-Charles de Gaulle, Seychelles, Yaounde, Zanzibar |
Linhas Aéreas de Moçambique | Maputo, Pemba |
Marsland Aviation | |
Nasair | Asmara, Khartoum |
Precision Air | Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Shinyanga, Zanzibar |
Qatar Airways | Doha |
Rwandair Express | Kigali |
Saudi Arabian Airlines | Jeddah, Johannesburg |
South African Airways | Johannesburg |
Sudan Airways | Khartoum |
Swiss International Air Lines | Zürich |
Turkish Airlines | Istanbul-Atatürk |
Virgin Atlantic | London-Heathrow |
Ndege za shehena
[hariri | hariri chanzo]- Air
- Cargolux
- EgyptAir Cargo
- Evergreen International Airlines
- Kenya Airways Cargo
- Lufthansa Cargo
- Martinair Cargo
- Simba Air Cargo
- Singapore Airlines Cargo
Ajali na matukio
[hariri | hariri chanzo]- Tarehe 20 Novemba 1974, ndege ya Lufthansa Flight 540 Lufthansa Boeing 747-130, D-ABYB, LH 540,"Hessen" (Jimbo la Kijerumani)iliyoundwa mwaka wa 1970, ilipata ajali wakati wakutia nang'a katika ujia wa 24 mjini Nairobi.Iliwauwa watu 59 kati ya 157 waliokuwemo ndani. Ndege hiyo ilikuwa imeondoka Frankfutt ikielekea Johannesburg kupitia Nairobi.
- Mei mwaka wa 1989 ndege moja ya Boeing 707-330B ndege ya Huduma za ndege za Somali(Somali Airlines)ilipoteza mwelekeo katika ujia wake na kuanguka katika shamba moja karibu na uwanja wa ndege. Ndege yenyewe ilikuwa na watu 70, lakini hakuna vifo wala maumivu yoyote yaliyoibuka.
- Tarehe 4 Desemba,mwaka wa 1990, ndege aina ya Boeing 707-321C inayomilikiwa na Sudania Air Cargo ilianguka karibu na uwanja wa ndege wakati wa kutua. Wote watu kumi waliokuwemo waliaga.
- Tarehe 30 Januari 2000, ndege ya Kenya Airways Flight 431 iliyotarajiwa kusafiri kutoka Nairobi hadi Lagos kisha baadaye hadi Abijan,ilibadilishiwa njia na kutua mjini Abijan. Ndege hiyo iligusa maji wakati wa kung'oa nanga uwanjani Lagos.
- Tarehe 5 Mei 2007, ndege ya Kenya Airways Flight KQ 507, kutoka Douala, nchi ya Cameroon iliripotiwa kupotea na abiria 115 na wahudumu wake. Hakuna manusura waliopatikana baada ya ndege hiyo kupatikana karibu na Douala nchini Cameroon.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Viwanja vya Ndege vya Nairobi
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Kenya Airports Authority - Jomo Kenyatta International Airport
- Airport information for HKJK at World Aero Data. Data current as of October 2006.
- Current weather for HKJK at NOAA/NWS
- Accident history for NBO at Aviation Safety Network