Precision Air

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Nembo ya Precision Air

Precision Air ni ndege iliyo na makao yake mjini Dar Es Salaam nchini Tanzania. Inahudumia watalii na wafanyibiashara wanaosafiri kwenye viwanja vya ndege 10 nchini Tanzania, pamoja na ndege za kwenda nchi ya Kenya na Uganda. Makao yake makuu ni kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, mjini Dar es Salaam na ikiwa na vituo kwenye viwanja vya ndege vya Kilimanjaro, Arusha na Mwanza.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Precision Air ilianzishwa mnamo 1991 na kuanza huduma mnamo 1994. Hapo awali, kampuni hii ilikuwa ya kibinafsi, lakini Kenya Airways ilinunua 49% kwa $ milioni 2, wiki chache tu baada ya South African Airways iliponunua 49% ya Air Tanzania. Asilimia 51 iliyobaki ilikuwa ni ya Michael Ngaleku Shirima.[1] /Kuanzia October 2011,Precision Air iliamua kuanza kuuza hisa zake katika soko la hisa la Dar es salaam na hivyo umilika wa Michael Shirima na Kenya Airways utapungua mpaka asilimia 33 kila moja.

Baada ya kuanza kuuza hisa zake kwa umma, Michael Shirima alitoa nusu ya hisa zake na Kenya Airways wakatoa nusu ya hisa zao. Kwa hivyo theluthi moja ya hisa hizo itamilikiwa na umma. Bei ya hisa moja inauzwa kwa Shilingi 475.

Miji inayosafiria[hariri | hariri chanzo]

Precision Air nchini Kenya.

Precision Air inasafiri hadi miji ya Dar es Salaam, Arusha, Kigoma, Kilimanjaro, Musoma, Mwanza, Shinyanga, Tabora, Zanzibar, Mombasa, Nairobi na Entebbe.[Johanesburg][Hahaya][Bukoba] Mkakati wa kwenda katika maeneo mengine bado upo

Ndege zake[hariri | hariri chanzo]

Hadi 26 Agosti 2009, Precision Air ina ndege zifuatazo:

  • Ndege 4aina ya ATR42-400'
  • Ndege 5 aina ya ATR 72-500
  • Ndege 2 aina ya Boeing 737-300

Zilizowekwa oda[hariri | hariri chanzo]

  • Ndege 2 aina ya ATR 42-500
  • Ndege 1 aina ya ATR 72-500
  • Majina ya ndege hizo ni 5HPAA,5HPAG,5HPWE na 5HPWF ambazo ni ATR42
  • Nyingine ni 5HPWA,5HPWB,5HPWC,5HPWD na 5HPWG ambazo ni ATR72
  • Vile vile wana BOEING 737-300 mbili ambazo ni 5HPAZ na 5HPMS

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]