Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Murtala Muhammed

Majiranukta: 06°34′38″N 003°19′16″E / 6.57722°N 3.32111°E / 6.57722; 3.32111
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Murtala Muhammed


06°34′38″N 003°19′16″E / 6.57722°N 3.32111°E / 6.57722; 3.32111 Kigezo:Infobox airport

Uwanja wa Ndege Kimataifa wa Murtala Muhammed (Murtala Muhammed International Airport kwa lugha ya kimombo) uko katika sehemu ya Ikeja, nchi ya Lagos, nchini Nigeria, na uwanja huu wa ndege ndio ambao unahudumia mji [1]wa Lagos, kusini magharibi mwa Nigeria na taifa zima. Awali uwanja huu wa ndege ulikuwa unajulikana kama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Lagos (Lagos International Airport kwa Kiingereza), lakini jina lake lilibadilishwa ujenzi ulipofikia katikati kuwa Murtala Muhammed ambaye alikuwa mkuu wa zamani wa kijeshi wa Nigeria. Taminalii ya kimataifa ilijengwa kama ya Uwanja wa ndege wa Schiphol iliyoko mjini Amsterdam. Uwanja huu wa ndege ulifunguliwa rasmi tarehe 15 Machi 1979. Uwanja huu ndio wigo kuu kwa ndege kama vile flag carrier airlines ya Nigeria , Nigeria Eagle Airlines na Arik Air.

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Murtala Muhammed ina taminali ya kimataifa na ya taifa (domestic), ambazo zimetenganishwa na umbali wa kilomita moja. Taminali zote zinatumia barabara moja pamoja Taminali ya Taifa ilihamishwa na kupelekwa katiak Taminali ya taifa ya kitambo Lagos mwaka wa 2000 baada ya moto. Taminali mpya ya Taifa ilijengwa na na kupitishwa na tume mnamo 7 Aprili 2007.

Mwaka 2008, uwanja huu wa ndege uliwahudumia abiria 5,136,697.

Historia na sifa[hariri | hariri chanzo]

Katika mwishoni mwa miaka ya 1980 na ya 1990, taminali ya kimataifa ilikuwa na sifa mbaya ya kuwa uwanja wa ndege ambao ni hatari. Kutoka mwaka wa 1992 hadi mwaka wa 2000, US Federal Aviation Administration ilivionya viwanja vya kimataifa vya ndege vya Marekani kwa kuwashauri abiria kwamba hali ya usalama katika LOS haikufikisha yaliyokuwa yanahitajika na ICAO. Mwaka 1993 FAA ilipiga marufukuhuduma za ndege kati ya Lagos na Marekani. Katika kipindi hicho, usalama katika LOS uliendelea kuwa tatizo kubwa. Abiria waliokuwa wakiwasili mjini Lagos walikuwa wanasumbuliwa ndani na nje ya uwanja wa ndege na wahalifu. Wafanyakazi wa uwanja wa ndege walichangia sifa yake. Maafisa wa uhamiaji waliitisha rushwa kabla ya kupiga chapa pasi, na wakati huo huo mawakala wa forodha walidai malipo ya ada ambayo hayakuwepo. Aidha, aina ya ndege ya jet kadhaa zilishambuliwa na wahalifu ambao walikuwa wanasimamisha ndege zilizokuwa zinawasafirisha abiria kutoka na kwenda kwa taminali kisha kuiba mizigo yao. Waongozi wasafiri walipendekeza kuwa abiria wa Nigeria wapitie Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Mallam Aminu Kano katika eneo la Kano na kuchukua ndege za ndani au kusafiri kutumia barabara hadi Lagos.


Kufuatia uchaguzi wa kidemokrasia wa Olusegun Obasanjo mwaka wa 1999, hali ya usalama katika LOS ilianza kuboreka. Polisi wa uwanja wa ndege waliweka sera la " shoot on sight "ambayo inamaanisha kupiga mhalifu kutumia risasi iwapo mtu yeyote atakaye patikana katika maeneo ya usalama kuzunguka barabara ya ndege na sehemu za teksi. Polisi walilinda ndani ya taminali na maeneo ya kuwasili ya nje. FAA iliondoa marufuku ya huduma ya moja kwa moja kwenda Nigeria mwaka wa 2001 katika utambuzi wa maboresho haya ya usalama.


Miaka ya hivi karibuni tumeona marekebisho katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Murtala Muhammed. Miundombinu zisizofanya kazi na zisizoendeshwa kama vile viyoyozi na vifaa vya kubeba mizigo ya abiria vimerekebishwa. Uwanja nzima wa ndege umesafishwa, mikahawa na maduka yamefunguliwa. Makubaliano ya huduma za anga kati ya Nigeria na nchi nyinginezo vinafufuliwa na vipya vinatiwa saini. Makubaliano haya yameonyesha hisia na haki za kutua kutoka kwa Emirates, Ocean Air Delta na China Southern Airlines katika uwanja wa ndege wa kimataifa kubwa zaidi nchini Nigeria.


Serikali ya Shirikisho imewapa kibali kwa ajili ya upanuzi wa ukumbi wa kuondoka na kuwasili wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Murtala Muhammed ili kupunguza trafiki inayozidi katika uwanja huo wa ndege.

Takwimu[hariri | hariri chanzo]

Takwimu ya Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Murtala Muhammed
mwaka Jumla ya Abiria Asilimia ya ongezeko Mizigo(tani) Jumla ya ndege
2003 3.362.464 -% 51.826 62.439
2004 3.576.189 6. 89.496 67.208
mwaka wa(2005). 3.817.338 6.3% 63.807 70.893
2006 3.848.757 0,8% 83.598 74.650
2007 4,162,424 [2] 7.5%
2008 5,136,697 [2] 23.5%

Ndege na Sehemu za Usafiri[hariri | hariri chanzo]

Taminali 1 (Kimataifa)[hariri | hariri chanzo]

Makampuni ya ndege Vifiko 
Aero Contractors Accra
Afriqiyah Airways Cotonou, Tripoli
Air France Paris-Charles de Gaulle
Air Ivoire Abidjan, Douala
Alitalia Rome-Fiumicino
Arik Air Accra, Banjul, Cotonou, Dakar, Freetown, Johannesburg, London-Heathrow, New York-JFK
British Airways London-Heathrow
China Southern Airlines Beijing-Capital, Dubai
Delta Air Lines Atlanta
EgyptAir Cairo
Emirates Dubai
Ethiopian Airlines Accra, Addis Ababa
Iberia Airlines Madrid
Kenya Airways Nairobi
KLM Amsterdam
Lufthansa Frankfurt
Middle East Airlines Beirut
Nigerian Eagle Airlines Abidjan, Accra, Banjul, Cotonou, Dakar, Douala, Libreville, Monrovia
Qatar Airways Doha
Royal Air Maroc Casablanca
South African Airways Johannesburg
Turkish Airlines Istanbul-Atatürk
United Airlines Washington-Dulles [begins 3 Mei][3]
Virgin Atlantic London-Heathrow

Taminali 2 (Ndani au Taifa ukipenda)[hariri | hariri chanzo]

Makampuni ya ndege Vifiko 
Aero Contractors Abuja, Benin City, Calabar, Enugu, Jos, Kaduna, Owerri, Port Harcourt, Warri
Chanchangi Airlines Abuja, Kaduna, Owerri, Port Harcourt
Dana Air Abuja, Enugu, Kano, Port Harcourt
IRS Airlines Abuja, Kano, Maiduguri, Yola
Nigerian Eagle Airlines Abuja, Kano, Owerri, Port Harcourt, Sokoto

General Aviation Taminali (Ndani)[hariri | hariri chanzo]

Makampuni ya ndege Vifiko 
Arik Air Abuja, Akure, Benin City, Calabar, Enugu, Gombe, Ilorin, Jos, Kaduna, Kano, Maiduguri, Owerri, Port Harcourt, Sokoto, Uyo, Warri, Yola
Associated Aviation Benin City, Ibadan
Overland Airways Ibadan, Ilorin, Minna

Ndege za mizigo[hariri | hariri chanzo]

Makampuni ya ndege Vifiko 
Air France Cargo Ndjamena, Paris-Charles de Gaulle
Allied Air Ostend
Avient Aviation Abidjan, Bamako, Châlons-en-Champagne, Libreville, Malabo, Ouagadougou, Pointe-Noire, Port Harcourt, Sharjah
Cargolux Luxembourg
Jade Cargo Sharjah
Star Airlines (Macedonia) Skopje, Bishkek, Sharjah, Hong Kong

Ajali na matukio[hariri | hariri chanzo]

  • Tarehe 23 Novemba 1996, wateka nyara walililazimisha Ethiopia Airlines Flight 961, kutoka Mumbai na Addis Ababa likielekea Abidjan kupitia masimamo mengi (pamoja na Lagos), kupata ajali katika Bahari ya Hindi.
  • Tarehe 30 Januari 2000, Kenya Airways Flight 431 lililotarajiwa kutoka Nairobi hadi Lagos tena hadi Abidjan, lakini badala yake ndege lilielekea Abidjan. Ndege hiyo ilitumbukia majini baada ya kuondoka Lagos.
  • Tarehe 28 Novemba 2003, udhibiti wa Lagos ulikubali Hydro Air 501, ndege aina Boeing 747-200 kutoka Uwanja wa ndege wa Brussels kutua katika Runway 19R. Ndege hiyo iligonga jiwe, kisha ikaelekea upande wa kushoto na injini yake ya kwanza huku ikigusana na jiwe hilo hadi “nosewheel” ikatua kwenye mtaro. Ripoti ya Wizara ya Ndege ilihitimisha kuwa sababu ya ajali ya ndege ilikuwa kwamba ndege ilipewa kibali cha kutua katika Runway ambao ilifaa kuwa imefungwa.
  • Tarehe 22 Oktoba 2005, Bellview Airlines Flight 210, ilifaa kutua mjini Abuja, ilipata ajali baada ya kuondoka, na kuwaua watu wote waliokuwa ndani.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named FAAN
  2. 2.0 2.1 "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-15. Iliwekwa mnamo 2023-07-01. 
  3. http://www.united.com/press/detail/0,7056,61241,00.html

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]