Mumbai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mumbai

Mumbai (Kihindi: मुंबई  pia: Bombay) ni mji mkuu wa jimbo la Maharashtra kwenye pwani la magharibi la Uhindi. Mumbai ni mji mkubwa wa India mwenye wakazi milioni 12.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mji ulianzishwa kwenye kisiwa kilichopo karibu sana na bara. Kitovu kipo kwenye rasi inayoelekea katika Bahari Hindi. Kisiwa kilinunuliwa na Wareno mwaka 1534 nao Wareno waliwakabidhi kisiwa kwa Uingereza 1661.

Mji uliendelea kuwa bandari kuu ya Waingereza katika Uhindi ukakua. Mwaka 1852 reli ya kwanza ya Asia ilianzishwa hapa. Tangu siku za Wareno mji uliitwa Bombay lakini sehemu ya wenyeji waliona ni jina la kikoloni.

1995 serikali ya Maharashtra iliamua kubadilisha jina kuwa Mumbai kwa heshima ya mungu mmoja wa Kihindu. Wenyeji wanaendelea kutumia majina yote mawili.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Mumbai-Bombay ni kitovu cha filamu nchini Uhindi kwa kutania imeitwa mara nyingi "Bollywood". Ni mji muhimu wa viwanda na biashara. Bandari yake inashughulika asilimia 40 ya biashara ya nje ya taifa.

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mumbai kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.