Bollywood
Bollywood (Kihindi: बॉलीवुड, Kiurdu: بالی وڈ) ni neno la kutaja tasnia ya filamu za lugha ya Kiurdu-Kihindi huko nchini India.[1]
Chimbuko
[hariri | hariri chanzo]Kwa ujumla hutajwa kama Sinema za Kihindi, lakini hiyo si sahihi. Bollywood hutaja filamu za lugha ya Kihindi tu, basi. Istilahi ya Bollywood inaunganisha Bombay na Hollywood (ambapo filamu nyingi za Kimarekani zinatengenezwa).
Dhumuni
[hariri | hariri chanzo]Bollywood hutengeneza filamu nyingi sana kwa mwaka. Filamu nyingi za Bollywood huitwa Masala. Kwa Kihindi, Masala ina-maana ya viungo. Filamu hizi huwa na kiwango cha juu sana cha kimahaba, visasi, na hali ya utajiri na umaskini ndani yake.
Lugha zinazotumika kwenye filamu za Bollywood
[hariri | hariri chanzo]Filamu zinazotayarishwa Bollywood kwa kawaida huwa kwa lugha ya Kihindi. Hindustani, sehemu mashuhuri kote kwa Kihindi na Kiurdu. Bollywood hutengeneza filamu zake kwa lugha ya Kihindi, Urdu na Kiingereza.
Badiliko
[hariri | hariri chanzo]Mtahakiki wa filamu Lata Khubchandani ameandika,"..filamu zetu za awali...(zilikuwa)na uhuru wa sehemu za kubusiana na mapenzi ndani yake. Cha-kushangaza, ilikuwa baada ya Uhuru bodi ya sensa imeingilia kati na ikabadilisha kila kitu."[2]
Waongozaji wa filamu
[hariri | hariri chanzo]- Sanjay Leela Bhansali
- Farah Khan
- Karan Johar
- Yash Chopra
- Ashutosh Gowariker
- Satish Kaushik
- Mani Ratnam
- Aditya Chopra
historyczni
Wanakoreografia
[hariri | hariri chanzo]Waigizaji wa kike
[hariri | hariri chanzo]Waigizaji wa kiume
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-15. Iliwekwa mnamo 2016-05-10.
- ↑ Free Reeling,PLAY, Sunday Mid-day , 11 Machi 2007, Mumbai.MH/MR/WEST/66/2006-08 Khubchandani, Lata. "Memories of another day". mid-day.com.
Viungo ya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Bollypedia Ilihifadhiwa 12 Novemba 2010 kwenye Wayback Machine. (Kijerumani)
- Bollywood.pl Ilihifadhiwa 26 Oktoba 2010 kwenye Wayback Machine. (Kipoland)
- eBollywood - Twoja Kraina Marzeń Ilihifadhiwa 7 Septemba 2011 kwenye Wayback Machine. (Kipoland)