Nenda kwa yaliyomo

Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ukumbi wa KICC

Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta au Kenyatta International Conference Centre (KICC) ni jengo la ghorofa 30 iliko mjini Nairobi, Kenya.

Iko katikta eneo la kati la biashara la Nairobi. Ni ukumbi kwa mikutano, maonyesho na matukio maalumu ndani ya umbali wa kutembea wa hoteli kadhaa za nyota tano. Imekuwa mwenyeji wa mikutano mingi ya kimataifa na semina.

Kuna vyumba kadhaa vya mikutano vilivyo na vifaa vizuri na kile kikubwa kabisa kiko na uwezo wa zaidi ya wajumbe 4,000. Iko na vifaa vya kutafsiria lugha sambamba ambavyo vina uwezo wa kutafsiria lugha saba, kituo cha biashara cha kisasa, benki, huduma za ziara na kusafiri, kiwanja kikubwa na pahali pa kuegezea magari salama.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta ulijengwa kati ya miaka ya 1966-1973. Ilifadhiliwa na serikali. Mwaka 1989 umiliki wake uli kwa chama cha kisiasa cha KANU, chama cha kisiasa cha kisheria pekee nchini Kenya. KICC ilirejeshwa kwa serikali mwaka 2003, wakati KANU walitolewa kwa serikali [1]

Jumba la Amphitheatre

[hariri | hariri chanzo]

Katika jumba la amphitheatre "urithi na usasa wakutana". Liliundwa kwa mikutano ya ukubwa wa kati, viti 800 katika balcony tatu zilizozunguka auditorium, huleta uhai katika mikutano yoyote ya kibiashara. Iko na vibanda vya SIE, vifaa kamili vya mantiki za kurekodi, vifaa vya hali ya juu vya kutangazia umma na vya kuzuia sauti.

Jumba la Mjadala

[hariri | hariri chanzo]

Kama jumba kubwa zaidi la mikutano la aina yake katika Afrika ya Mashariki, jumba hili limezungukwa na mawe ya kuzuia sauti, mbao asili na dari la kifahari. Jumba hili huhudumia mikutano mikubwa ya kimataifa, maonyesho na sherehe kubwa za kifahari, na lina uwezo wa watu 5,000. Liko na vifaa vya hali ya juu vya kurekodia na kupazia sauti, vibanda visivyotumia waya vya kutafsiria (hadi lugha saba) na maeneo ya kuangalilia. Dari zake za juu ziliwekwa kwa sababu ya mapambo mazuri, bendera za kukuza na nyenzo zingine za kukuza.

Hili ni ua la mita mraba 705 lililo na lami linalozunguka sanamu ya Jomo Kenyatta. Liliundwa kama eneo la mapumziko kwa wale wanaohudhuria mikutano. Ua hili liko na bustani, vidimbwi vya maji na chemichemi. Fito kadhaa za bendera na mabalcony uani zimetengenezwa na fashoni ambayo huziwezesha kuhudumia makutio ya kukuzia.

Uwanja wa COMESA

[hariri | hariri chanzo]

Uwanja huu wa COMESA ni mkubwa na uko kando na bunge la Kenya. Mwaka 1999, onyesho kubwa zaidi kufanyika nchini Kenya, lililowaleta pamoja waonyeshi wa COMESA kutoka kila nchi, lilifanyika KICC. Miongoni mwa waliohudhuria walikuwa wakuu tisa wa nchi, waliokuja kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi. Uwanja huu unaweza kutumiwa kuhudumia maonyesho makubwa ama kuegeshea magari hadi 1,000.

  1. [1] ^ Daily Nation, 11 Novemba 2003: Jitihada za KANU za kuimiliki KICC tena zakosa kufanikiwa

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]