Hema

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mji wa hema za wapenzi wa muziki waliokuja kwa tamasha za bendi
Muundo wa hema sahili

Hema ni kibanda chepesi kinachofanywa na kiunzi cha ndani na ganda la nje la kitambaa, plastiki au ngozi. Kazi yake ni kukinga dhidi ya jua, mvua, baridi au athira nyingine za hali ya hewa. Hema ni rahisi kufumuliwa na kupelekwa mahali pengine kwa matumizi mapya.

Katika jamii zinazofuata maisha ya uhamaji hema ni kawaida badala ya nyumba imara, kwa mfano wafugaji wanaohamahama pamoja na kondoo, mbuzi, ng'ombe au ngamia zao.

Mahema madogo yanatumiwa pia kama kinga ya muda kwa burudani kama camping au matembezi marefu. Mahema makubwa zaidi hutumiwa na jeshi kwa kambi za muda, pia wakati wa maafa kama watu hawana nyumba tena: kwa mfano baada ya tetemeko la ardhi au mafuriko. Mahema makubwa sana zatumiwa kwa mikutano mahali pasipo ukumbi mkubwa kiasi cha kutosha.

Picha za hema[hariri | hariri chanzo]