Kipululu
Mandhari
(Elekezwa kutoka Kiunzi)
-Kwa kiunzi cha binadamu tazama makala "Kiunzi cha mifupa"-
Kipululu | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kipululu wa Afrika (Turnix sylvaticus lepurana)
| ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Jenasi 2, spishi 17:
|
Vipululu (pia vipururu) ni ndege wa familia Turnicidae. Spishi moja inaitwa kiunzi pia (tazama orodha ya spishi). Ndege hawa wanafanana tombo lakini hawana mnasaba na hawa. Wana rangi ya mchanga na madoa meusi au kahawia. Hawapendi kupuruka. Jike ana rangi kali kuliko dume na huanzisha ubembelezi. Dume huatamia na hutunza makinda.
Ndege hawa waliainishwa zamani ndani ya Gruiformes (oda ya makorongo) au Galliformes (oda ya kuku). Lakini utafiti wa ADN umeonyesha kama vipululu wana mnasaba na vitwitwi. Kwa hivyo wanaainishwa ndani ya Charadriiformes sasa. Kisukuku kimefunuliwa ambacho kimetambuliwa kama jamaa wa vipululu na kuitwa Turnipax.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Ortyxelos meiffrenii, Kiunzi (Quail-plover au Lark buttonquail)
- Turnix hottentottus, Kipululu Kusi (Hottentot buttonquail)
- Turnix nanus, Kipululu Kiuno-cheusi (Black-rumped buttonquail)
- Turnix nigricollis, Kipululu wa Madagaska (Madagascar buttonquail)
- Turnix sylvaticus, Kipululu wa Kawaida (Common buttonquail)
- Turnix s. lepurana, Kipululu wa Afrika (African hemipode
- Turnix s. sylvaticus, Kipululu wa Maroko (Andalusian hemipode
Spishi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Turnix castanotus (Chestnut-backed buttonquail)
- Turnix everetti (Sumba buttonquail)
- Turnix maculosus (Red-backed buttonquail)
- Turnix melanogaster (Black-breasted buttonquail)
- Turnix ocellatus (Spotted buttonquail)
- Turnix olivii (Buff-breasted buttonquail)
- Turnix pyrrhothorax (Red-chested buttonquail)
- Turnix suscitator (Barred buttonquail)
- Turnix sylvaticus (Common buttonquail)
- Turnix tanki (Yellow-legged buttonquail)
- Turnix varius (Painted buttonquail)
- Turnix velox (Little buttonquail)
- Turnix worcesteri (Worcester's au Luzon buttonquail)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Kiunzi
-
Kipululu wa Madagaska
-
Sumba buttonquail
-
Red-backed buttonquail
-
Black-breasted buttonquail
-
Barred buttonquail
-
Yellow-legged buttonquail
-
Painted buttonquail