Nenda kwa yaliyomo

Kipululu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

-Kwa kiunzi cha binadamu tazama makala "Kiunzi cha mifupa"-

Kipululu
Kipululu wa Afrika (Turnix sylvaticus lepurana)
Kipululu wa Afrika (Turnix sylvaticus lepurana)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Charadriiformes (Ndege kama vitwitwi)
Familia: Turnicidae (Ndege walio na mnasaba na vipululu)
Ngazi za chini

Jenasi 2, spishi 17:

Vipululu (pia vipururu) ni ndege wa familia Turnicidae. Spishi moja inaitwa kiunzi pia (tazama orodha ya spishi). Ndege hawa wanafanana tombo lakini hawana mnasaba na hawa. Wana rangi ya mchanga na madoa meusi au kahawia. Hawapendi kupuruka. Jike ana rangi kali kuliko dume na huanzisha ubembelezi. Dume huatamia na hutunza makinda.

Ndege hawa waliainishwa zamani ndani ya Gruiformes (oda ya makorongo) au Galliformes (oda ya kuku). Lakini utafiti wa ADN umeonyesha kama vipululu wana mnasaba na vitwitwi. Kwa hivyo wanaainishwa ndani ya Charadriiformes sasa. Kisukuku kimefunuliwa ambacho kimetambuliwa kama jamaa wa vipululu na kuitwa Turnipax.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]