Ngong, Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ngong, Kenya ni kusini magharibi ya Nairobi, karibu Bonde la Ufa (bofya ramani kulia)

Ngong ni mji iliyo karibu na Ngong Hills sambamba na Bonde la Ufa, iko katika kusini magharibi ya Nairobi, kusini mwa Kenya. Neno "Ngong" ni neno la kimaasai maana "nguyu" [1] kutokana na vilele vinne vya ushi, ambayo inasimama peke kutoka eneo tambarare la Nairobi. Vilima vya ngong, kutoka mteremko wa mashariki, zaangalia mbuga ya kitaifa ya Nairobi, na kaskazini mwa mji wa Nairobi. Vilima vya ngong, kutoka mteremko wa magharibi, zaangalia bonde la ufa fiti 4000 chini, ambapo vijiji vya Wamaasai vimekua vikiendelezwa.

Idadi ya jumla ya Ngong, nchini Kenya ni watu 57483, na mwinuko wa Ngong ni mita 1961 katika urefu, lakini urefu wa milima ni kama mita 2460 juu ya usawa wa bahari. [2] Ngong ni mji wa kati wa divisheni ya Ngong Wilaya ya Kajiado.

Katika miaka ya utawala wa ukoloni wa Uingereza, eneo kuzunguka vilima vya ngong ilikua sehemu ya kilimo ya walowezi, nyumba nyingi za jadi za ukoloni bado zinaonekana katika eneo hilo.


Ngong divisheni ina vitongoji vya Nairobi kama Ongata Rongai, Kiserian, Matasia na Kitengela ambapo wakazi ambao kimsingi ni wa Nairobi hujenga nyumba katika mikoa ya utulivu zaidi ya mji.

Katika filamu ya 1985 Out of africa, vilele vinne vya Ngong hutokea katika usuli kadhaa karibu na nyumba ya Karen Blixen's . Bado wakazi wa mitaa huripoti kuona simba katika vilima wakati wa miaka ya 1990.

Kaburi la wapweke la Denys Finch Hatton, iliyo na alama ya obelisk na bustani, iko kwenye mteremko wa mashariki wa vilima vya Ngong , inayoelekea hifadhi kubwa ya mbuga.

Vidokezo[hariri | hariri chanzo]

  1. ^ "FOUR DAYS - OLOGASAILE / MAGADI(BEAS 08)" (tour), Government of Kenya, 2006, BreakawayExpedition.com webpage: BreakawayExpedition-Tour.
  2. "Ngong, Kenya Page" (statistics), Falling Rain Genomics, Inc., 2004, FallingRain.com webpage: FallingRainCom-Ngong.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]