Eneo bunge la Dagoretti Kusini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jamhuri ya Kenya

Makala hii imepangwa kwa mfululizo:
Siasa na serikali ya
Kenya



Nchi zingine · Atlasi


Eneo bunge la Dagoretti Kusini ni jimbo la uchaguzi nchini Kenya, moja kati ya majimbo kumi na saba ya Kaunti ya Nairobi.

Awali liliitwa Eneo bunge la Dagoretti na lilikuwa mojawapo wa maeneo bunge ya Mkoa wa Nairobi. Lilijumuisha vitongoji vya magharibi vya Nairobi. Eneo Bunge la Dagoretti lilikuwa na mipaka sawia na tarafa ya Dagoretti ya Nairobi. Eneo lote la bunge hili lilikuwa katika eneo la Baraza la Mji wa Nairibi, likiwa na ukubwa wa eneo wa kilomita mraba 39.

Lilikuwa linajulikana kama Eneo Bunge la Nairobi West katika uchaguzi wa mwaka wa 1963, lakini jina lake lilibadilishwa kuanzia uchaguzi wa 1969.

Wabunge[hariri | hariri chanzo]

Mwaka wa Uchaguzi Mbunge [1] Chama Vidokezo
1963 Njoroge Mungai KANU
1969 Njoroge Mungai KANU Mfumo wa Chama kimoja.
1974 Johnstone Muthiora KANU Mfumo wa Chama kimoja. Muthiora punde baada ya kuchaguliwa [2].
1975 Francis Kahende KANU Uchaguzi mdogo, Mfumo wa Chama kimoja.
1979 Njoroge Mungai KANU Mfumo wa Chama kimoja.
1983 Clement Gachanja KANU Mfumo wa Chama kimoja.
1988 Chris Kamuyu KANU Mfumo wa Chama kimoja.
1992 Chris Kamuyu FORD-Asili
1997 Beth Wambui Mugo Social Democratic Party
2002 Beth Wambui Mugo NARC
2007 Beth Wambui Mugo Party of National Unity (PNU)

Kata na idadi ya watu[hariri | hariri chanzo]

Kata
Kata Idadi ya Watu*
Kawangware 86,824
Kenyatta/Golf course 30,253
Mutuini 14,521
Riruta 65,958
Uthiru/Ruthimitu 23,016
Waithaka 19,937
Jumla 240,081
Sensa ya 1999.
Wadi
Wadi Wapiga kura waliosajiliwa
Kawangware 22,662
Kenyatta/Golf course 24,948
Mutuini 6,344
Riruta 20,329
Uthiru/Ruthimitu 8,120
Waithaka 6,952
Jumla 89,355
*Septemba 2005| [3].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Center for Multiparty Democracy: Politics and Paliamenterians in Kenya 1944-2007 Archived 28 Februari 2008 at the Wayback Machine.
  2. Daily Nation, August14, 2003: Debate on PM is as old as Kenya
  3. Electoral Commission of Kenya: Registered voters per polling station by electoral area/ward and constituency

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]