Bunge la Afrika Mashariki

Bunge la Afrika Mashariki (kwa Kiingereza: East African Legislative Assembly, kifupi: EALA) ni chombo cha Jumuia ya Afrika Mashariki kwa kutunga sheria. Wabunge wanahudumu kwa miaka mitano.[1]
Bunge lilianzishwa tarehe 30 Novemba 2001.
Bunge la nne lina wajumbe 62, yaani 9 kwa kila nchi mwanachama, wakichaguliwa na bunge la nchi husika namna ya kuwakilisha kweli taifa lote, na wengine 8 kutokana na wadhifa wao. Spika ni Martin Ngoga kutoka Rwanda.
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |