Nenda kwa yaliyomo

Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Jumuiya Yetu)
Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Jumuiya Yetu au Wimbo wa Jumuiya Afrika Mashariki (kwa Kiingereza: EAC Anthem) ni wimbo wa taifa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Jina linatokana na maneno ya kwanza ya kiitikio yake.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Jumuiya Yetu iliumbwa tarehe 3 Desemba 2010 katikaMkutano wa 12 wa marais ya JAM (12th Ordinary Summit of the EAC Head of State), mjini Arusha.

Maneno ya Kiswahili Maneno ya Kiingereza
Ee Mungu twaomba uilinde
Jumuiya Afrika Mashariki
Tuwezeshe kuishi kwa amani
Tutimize na malengo yetu.
Kiitikio:
Jumuiya Yetu sote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu.
Uzalendo pia mshikamano
Viwe msingi wa Umoja wetu
Na tulinde Uhuru na Amani
Mila zetu na desturi zetu.
Kiitikio:
Jumuiya Yetu sote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu.
Viwandani na hata mashambani
Tufanye kazi sote kwa makini
Tujitoe kwa hali na mali
Tuijenge Jumuiya bora.
Kiitikio:
Jumuiya Yetu sote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu.
Oh God we pray
For preservation of the East African Community
Enable us to live in peace
May we fulfill our objectives
Chorus:
We should protect our community
We should be committed and stand strong
Our unity is our anchor
Long live our community.
Patriotism and togetherness
Be the pillars of our unity
May we guard our independence and peace
Our culture and traditions.
Chorus:
We should protect our community
We should be committed and stand strong
Our unity is our anchor
Long live our community.
In industries and in farms
We should work together
We should work hard
We should build a better community.
Chorus:
We should protect our community
We should be committed and stand strong
Our unity is our anchor
Long live our community.
  • Video ya Jumuiya Yetu
  • MINJA, Rasul Ahmed et RAMADHANI, Lupa. Ongezeko la Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki: Manufaa na Changamoto. 2018.