Nenda kwa yaliyomo

Juba ya chini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Juba ya chini (Kisomali: Jubbada Hoose‎, Kiarabu: جوبا السفلى‎, Kiitalia: Basso Giuba) ni mkoa wa kiutawala (gobol) kusini mwa Somalia.[1]

Makao makuu yake yakiwa Kismayo, kwenye autonomous Jubaland.

Una misitu ya kijani na wanyama pori kama simba, twiga, viboko, mamba na fisi.

Juba ya kusini imepakana na Kenya, Mkoa wa Kisomali wa Gedo, Juba ya kati (Jubbada Dhexe), na Bahari ya Somalia. Mkoa huu umepewa jina kufuatia Mto Jubba unaopita katikati yake na kuishilia kwenye Bahari ya Somalia katika Goobweyn.  

Hifadhi ya taifa ya Lag Badana ipo katika Juba ya kusini

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kuanzia mwanzo wa historia mpaka karne ya 19, Juba ya chini imekua ikikaliwa na ukoo wa Hawiye claw ambao ndio wakaaji wakubwa kusini mwa. Ijapokua ,baadae katikati ya karne ya 20, fa,ilia chache za Darod zilianza kuishi katika mji wa Kismayo. Kufikia mwisho was karne ya 20, kama wageni, walikwisha anzisha sehemu ndogo za kibiashara. Mwanzoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe Somalia, Kismaio ikifahamika kama  Waamo ilikumbwa na uharibifu mkubwa miongoni mwa viongozi wa vikundi sana sana kati ya Hawiye na Darod kila mmoja akidai umiliki wa mikoa ya Juba ya chini na kati. Ila kwa upande mwingine, Mji ulikua kiuchumi kufikia kuwa eneo kubwa la biashara ya mifugo.[2] Wawakilishi wakuu kujianzisha kismayo walikua  Majeerteen wafanya biashara kutoka Kaskazini Ras Hafun wenye hadhi, waliotabulika kama Hafuuni. Katika miungo miwili ya kwanza ya karne ya 20, wakati wa upinzani wa Mohammed Abdullah Hassan ("Mad Mullah") Dervish wafuasi wa ukoo mdogo wa Dhulbahante walijiunga pia[3]

Miongoni mwa vitu vingi, mikoa yote inaonekena kukaliwa na familia zisizo za wakazi asili kuanzia mwanzo wa muundo shirikishi ndani ya nchi nzima.   Kati ya  1974 na 1975,ukame mkubwa uliojulikana kama Abaartii Dabadheer ("Ukame Lingering ") ulitokea  kaskazini mwa Nchi ya Somalia. Umoja wa Kisoviet, amboa kwa wakati huo ulikua na mahusiano ya kimkakati na  serikali ya the Siad Barre, uliwachukua watu wake wapatao  90,000 kutoka katika maeneo yaliyoharibiwa na ukame ya Hobyo na  Caynaba. Makazi mapya madogo yaliyojulikana kama Danwadaagaha ("makazi jumuishi") yalianzishwa katika mikoa ya Jubbada Hoose (Jubba ya chini) na Jubbada Dhexe (Jubba ya kati). Familia zilizosafirishwa walijuzwa juu ya njia za kilimo na uvuvi, mabadiliko kutoka kwenye njia zao za jadi za ufugaji na uchungaji wa mifugo.

Juba ya chini inaundwa na wilaya tano:[4]

Visiwa vya Bajuni vipo ndani ya mkoa huu pia.

Miji mikubwa

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Somalia". The World Factbook. Langley, Virginia: Central Intelligence Agency. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-07-01. Iliwekwa mnamo 6 Desemba 2013. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Lee V. Cassanelli, The shaping of Somali society: reconstructing the history of a pastoral people, 1600–1900, (University of Pennsylvania Press: 1982), p.102.
  3. Greenstone - Kismayo
  4. "Districts of Somalia". Statoids. Iliwekwa mnamo 6 Desemba 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Kigezo:Mikoa ya Somalia

Makala hii kuhusu maeneo ya Somalia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Juba ya chini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.