Nenda kwa yaliyomo

Kismayu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kismayo)


Kismayu
Kismayu is located in Somalia
Kismayu
Kismayu

Mahali pa mji wa Kismayu katika Somalia

Majiranukta: 0°21′37″N 42°32′56″E / 0.36028°N 42.54889°E / 0.36028; 42.54889
Nchi Somalia
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 183,300
Muonekano wa mji wa Kismaayo
Ramani

Kismayu (pia: Kismayo au kwa Kisomali: Kismaayo) ni mji katika mkoa wa Jubbada Hoose wa Somalia mwambaoni mwa Bahari Hindi. Uko karibu na mdomo wa mto Juba. Kismayu ndio mji mkubwa katika eneo la Jubbaland. Mji wenyewe uko km 528 kusini magharibi mwa mji mkuu Mogadishu.

Katika mwaka wa 2011, Kismayu ilikadiriwa kuwa na wakaazi 183,300[1].

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mji ulianzishwa na Wabajuni waliokuwa Waswahili Wabantu. Wasomali wenyewe walichelewa kufika eneo hili. Katika karne za kati, Kismayu ilikuwa chini ya serikali ya Ajuuraan iliyokuwa ikutawala eneo kadhaa za Somalia.

Kismayu pamoja na pwani ilikuwa chini ya masultani wa Zanzibar tangu 1835 BK. Kati ya 1875 na 1876 Kismayu ilitawaliwa na Misri.

Tangu 1895 ilikuwa chini ya utawala wa Uingereza pamoja na Kenya lakini mwaka 1924 ilikabidhiwa kwa utawala wa Italia. Ikawa mji mkuu wa jimbo la Oltre Giuba (ng'ambo ya Juba).

Kismayu iliharibika sana kutokana na mapigano katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Somalia tangu 1991.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "SOMALIA City & Town Population Geography Population Map cities coordinates location - Tageo.com". www.tageo.com. Retrieved 23 December 2016.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Somalia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kismayu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.