Shirikisho la Afrika Mashariki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani hii huonyesha kwa rangi ya kijani pendekezo la Shirikisho la Afrika Mashariki.

Shirikisho la Afrika Mashariki ni mpango wa kuanzisha shirikisho la kisiasa kati ya nchi saba zilizoko kwenye Jumuiya ya Afrika MasharikiBurundi, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda - kuwa nchi moja.[1]

Mwezi Septemba 2018 kamati iliundwa kuandika katiba ya Shirikisho la Afrika Mashariki.[2] Mwaka 2023 shirikisho hilo lilitariwa kuchukua nafasi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya sasa lakini inaonekana si rahisi kuwahi hivyo, ingawa hatua nyingi zimeshachukuliwa.[3][4]

Shida kubwa ni kwamba nchi hizo saba kwa kiasi tofauti zinaathiriwa na ufisadi, ukabila kama si vita vya wenyewe kwa wenyewe.[5] Hata hivyo, faida ya umoja inazisukuma kuungana.[6][7]

Vipengele vya Shirikisho[hariri | hariri chanzo]

Likiwa na kilometa za mraba 4,812,618, Shirikisho la Afrika Mashariki litakuwa nchi kubwa zaidi katika Afrika na ya saba katika dunia nzima. Kwa watu 281,050,447 katika mwaka 2022, litakuwa nchi kubwa zaidi katika Afrika na nchi ya nne katika dunia, baada ya China, India na Marekani.

Katika Shirikisho la Afrika Mashariki, Kiswahili kitakuwa lugha rasmi na Arusha makao makuu.

Mpango ni kuwa pesa ya Shirikisho la Afrika Mashariki itakuwa Shilingi ya Afrika Mashariki.[1] Ripoti ya 2013 ilisema kwamba itakuwa pesa ya nchi tano za Afrika Mashariki kufikia 2023.[8] Pato la ndani au GDP linakisiwa kuwa dola za Marekani bilioni 602.584, ya thelathini na nne katika dunia.[9]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Katika miaka ya 1960, karibu na wakati wa uhuru wa Kenya, Tanganyika, Uganda, na Zanzibar kutoka Uingereza, viongozi wa siasa wa nchi nne walikuwa na nia ya kuunda shirikisho. Mwaka 1960, Rais Julius Nyerere alitaka kuahirisha uhuru wa Tanganiyka ili nchi zote katika Afrika Mashariki kupata uhuru pamoja.[10]

Katika mwezi Julai 1963, Jomo Kenyatta alimtembelea Rais wa Tanganyika Nyerere na Rais wa Uganda Milton Obote.[10] Walikutana katika mji wa Nairobi. Walizungumza kuhusu uwezekano wa kuunganisha nchi zote na Zanzibar pamoja ili kuwa na nchi kubwa. Walikubaliana kukamilisha kabla ya mwisho wa 1963[11][12][13] na baada ya mkutano, kulikuwa na mazungumzo na mipango kuhusu kuanzisha shirikisho rasmi.

Kwa upande wa Kenyatta, bado kulikuwa na wasiwasi kidogo kuhusu shirikisho walilokusudia. Mwaka 1964 ulifika na shirikisho halikuwa limezaliwa bado.[11] Mwezi Mei 1964, Kenyatta alikataa kupokea azimio la kuanzisha shirikisho kwa haraka.[11] Alisema kwa uwazi kuwa mazungumzo ya shirikisho yaliambatana na ujanjaujanja wa kuharakisha uhuru wa Kenya, lakini hata hivyo Nyerere alikataa madai ya Kenyatta.[11] Karibu wakati huohuo, Obote alisema yeye hakupenda Shirikisho la Afrika Mashariki kwa sababu alipendelea kuwe na umajumui wa Afrika. Alisema hivi kwa sababu ya upinzani toka nchini kwake, hasa eneo la Buganda ambalo lilikuwa linajitegemea na ambalo halikupenda Shirikisho la Afrika Mashariki. Karibu na mwisho wa mwaka 1964, Shirikisho la Afrika Mashariki lilifariki ingawa Zanzibar na Tanganyika ziliunda shirikisho linaloitwa Tanzania.

Pendekezo la sasa[hariri | hariri chanzo]

Shirikisho la Afrika Mashariki lilizungumziwa tangu mwaka 2010 na lilikusudiwa kuanza kabla ya mwaka 2013.[14]

Katika mwaka 2010, Jumuiya ya Afrika Mashariki ilianzisha soko kwa bidhaa, huduma, ajira na mtaji katika Afrika Mashariki, na malengo yalikuwa kuwa na fedha moja kufikia mwaka wa 2013 na Shirikisho kamili kufikia mwaka 2015.[14]

Sudan Kusini ilikubaliwa kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika mwezi Machi 2016 na ilijiunga rasmi kama nchi ya sita katika mwezi Septemba 2016[15]. Kwa sasa Sudan Kusini inajenga bomba la mafuta litakaloungana na nchi ya Ethiopia na bandari ya Jibuti na pwani ya Kusini Mashariki mwa Kenya.[16] Bomba la mafuta katika Afrika Mashariki litatoa fursa kubwa kwa Sudan Kusini kuunganishwa na Shirikisho la Afrika Mashariki.[17]

Tarehe 14 Oktoba 2013, viongozi wa Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi walitembelea mji wa Kampala wakiwa na azma ya kuandika katiba ya Shirikisho la Afrika Mashariki.[18] Katika mwezi Desemba 2014, bidii ya kuanzisha Shirikisho la Afrika Mashariki ilisogezwa hadi 2016 au baadaye.[19]

Katika mwezi Desemba 2018, Jumuiya ya Afrika Mashariki ilikubali kuunda kamati ya kuandika katiba ya Shirikisho la Afrika Mashariki.[2]

Kamati hiyo ilikutana kwa mashauriano ya siku tano nchini Burundi kutoka 14-18 Januari 2020, ambapo ilitangaza kwamba katiba itaandaliwa mwishoni mwa mwaka 2021. Kufuatia idhini ya rasimu na majimbo sita ya EAC baada ya mwaka wa mashauriano, Shirikisho la Afrika Mashariki lingeanzishwa mwaka 2023. Njia ya kuelekea shirikisho kamili la kisiasa itajadiliwa kwa kina katika mikutano ya baadaye.

Tarehe 29 Machi 2022 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilikubaliwa kuwa nchi ya saba ya Jumuia hiyo.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

 1. 1.0 1.1 "Uganda Sunday Vision (2004-11-28): One president for EA by 2010". Sundayvision.co.ug. 28 November 2004. Archived from the original on 31 October 2012. Retrieved 15 July 2012.
 2. 2.0 2.1 "Ready for a United States of East Africa?". The East African (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-07-25. 
 3. "Overview of EAC". www.eac.int. Iliwekwa mnamo 2022-04-28. 
 4. "EAC Leadership". www.eac.int. Iliwekwa mnamo 2022-04-29. 
 5. "Explore the Map". Freedom House (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-29. 
 6. "President Uhuru Kenyatta calls for greater participation of youth in Africa in political and economic affairs". www.eac.int. Iliwekwa mnamo 2022-04-29. 
 7. "The African Executive | The Benefits of the East Africa Federation to the Youth". 2012-05-15. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 May 2012. Iliwekwa mnamo 2022-04-15.  More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); Check date values in: |archivedate= (help)
 8. "East African trade bloc approves monetary union deal", Reuters (kwa Kiingereza), 2013-11-30, iliwekwa mnamo 2019-07-25 
 9. "Report for Selected Countries and Subjects". www.imf.org. Iliwekwa mnamo 2019-07-25. 
 10. 10.0 10.1 "East African Federation", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2019-06-24, iliwekwa mnamo 2019-07-25 
 11. 11.0 11.1 11.2 11.3 Arnold, Guy. ([1974]). Kenyatta and the politics of Kenya. London,: Dent. ku. 173–174. ISBN 046007878X. OCLC 951249.  Check date values in: |date= (help)
 12. Assensoh, A. B. (1998). African political leadership : Jomo Kenyatta, Kwame Nkrumah, and Julius K. Nyerere. Malabar, Fla.: Krieger Pub. Co. uk. 55. ISBN 0894649116. OCLC 37457867. 
 13. Kyle, Keith (1997-12). "The politics of the independence of Kenya". Contemporary British History (kwa Kiingereza) 11 (4): 42–65. ISSN 1361-9462. doi:10.1080/13619469708581458.  Check date values in: |date= (help)
 14. 14.0 14.1 "The African Executive | The Benefits of the East Africa Federation to the Youth". web.archive.org. 2012-05-15. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-15. Iliwekwa mnamo 2019-07-25. 
 15. "South Sudan joins East African regional bloc". Daily Nation (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-07-25. 
 16. "South Sudan Oil Transit to Resume, Lamu Project will continue". GroundReport. 16 March 2012. Retrieved 15 July 2012.
 17. "EAC prepares to admit South Sudan". The East African (kwa Kiingereza). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-09-27. Iliwekwa mnamo 2019-07-25. 
 18. "Uganda hosts meeting of experts to fast-track political federation of East Africa - Sudan Tribune: Plural news and views on Sudan". www.sudantribune.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-10-22. Iliwekwa mnamo 2019-07-25. 
 19. "East Africa: Further Delays for the EAC Political Federation". 20 December 2014. Retrieved 4 May2015.