Kaunti ya Murang'a
- Kuhusu mji, soma Murang'a
Kaunti ya Murang'a | |||
---|---|---|---|
Kaunti | |||
Bunge la Kaunti ya Murang'a | |||
| |||
Murang’a County in Kenya.svg Kaunti ya Murang'a katika Kenya | |||
Nchi | Kenya | ||
Namba | 21 | ||
Ilianzishwa | Tarehe 4 Machi, 2013 | ||
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Kati | ||
Makao Makuu | Murang'a | ||
Miji mingine | Maragua, Kangema | ||
Gavana | Mwangi wa Iria | ||
Naibu wa Gavana | James Kamau Maina | ||
Seneta | Irungu Kang’ata | ||
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) | Sabina Wanjiru Chege | ||
Bunge la Kaunti | Bunge la Kaunti ya Murang'a | ||
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa | 35 | ||
Maeneo bunge/Kaunti ndogo | 7 | ||
Eneo | km2 2 524.2 (sq mi 974.6) | ||
Idadi ya watu | 1,056,640 | ||
Wiani wa idadi ya watu | 419 | ||
Kanda muda | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) | ||
Tovuti | murang'a.go.ke |
Kaunti ya Murang'a ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 1,056,640 katika eneo la km2 2,524.2, msongamano ukiwa hivyo wa watu 419 kwa kilometa mraba[1].
Makao makuu yako Murang'a.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Kaunti ya Murang'a imepakana na Nyeri (kaskazini), Embu, Machakos (mashariki), Kiambu (kusini) na Nyandarua (magharibi).
Kaunti hii iko kati ya m 914 na m 3353 juu ya usawa wa bahari wastani. Sehemu za magharibi zimekaribia Milima Aberdare na hivyo kuinuka zaidi. Ina mito kadhaa inayotiririka kutoka vitako vya Milima Aberdare kuelekea magharibi ambapo hutiririsha maji katika Mto Tana.
Murang'a ina vilima na mabonde ambayo huwezesha mito kutiririka. Topografia hii huwa na madhara wakati wa mvua kubwa kwa sababu ya mporomoko wa ardhi.
Udongo wa kaunti hii ni wa volkano ambao una rutuba inayowezesha kilimo. Murang'a huhusika katika kilimo cha kahawa, chai, ng'ombe wa maziwa na miti kama zao la biashara.
Murang'a ina maeneo matatu ya tabianchi:
- Msitu wa mvua wa tropiki, magharibi karibu na Milima Aberdare
- Nusutropiki, maeneo ya kati
- Nusuyabisi, mashariki
Utawala
[hariri | hariri chanzo]Kaunti ya Murang'a imegawiwa katika maeneo bunge yafuatayo:
Eneo bunge/kaunti ndogo | Kata |
---|---|
Kangema | Kanyenya-Ini, Muguru, Rwathia |
Mathioya | Gitugi, Kiru, Kamacharia |
Kiharu | Wangu, Mugoiri, Mbiri, Township, Murarandia, Gaturi |
Kigumo | Kahumbu, Muthithi, Kigumo, Kangari, Kinyona |
Maragua | Kimorori/Wempa, Makuyu, Kambiti, Kamahuhu, Ichagaki, Nginda |
Kandara | Ng'araria, Muruka, Kagundu-Ini, Gaichanjiru, Ithiru, Ruchu |
Gatanga | Ithanga, Kakuzi/Mitubiri, Mugumo-Ini, Kihumbu-Ini, Gatanga, Kariara |
Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [2]
[hariri | hariri chanzo]- Murang'a East 110,311
- Kangema 80,447
- Mathioya 92,814
- Kahuro 88,193
- Murang'a South 184,824
- Gatanga 187,989
- Kigumo 136,921
- Kandara 175,098
- Aberdare Forest 43
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kaunti ya Murang'a kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |