Papa Paskali I

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Paskali I.

Papa Paskali I alikuwa Papa kuanzia tarehe 25 Januari 817 hadi kifo chake mnamo Februari/Mei 824[1]. Alitokea Roma, Lazio, Italia[2].

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Paskali Massimi, mwana wa Bonosus[3].

Alimfuata Papa Stefano IV akafuatwa na Papa Eugenio II.

Kabla ya kuchaguliwa Papa alikuwa abati wa monasteri iliyohudumia waliofika mjini Roma kwa hija[4]. Kwa kuwa hakusubiri kupata uthibitisho wa kaisari Pius Mtawa, alimtuma balozi kwake[5] naye akarudi na hati Pactum cum Paschali pontifice, ambamo kaisari alimpongeza, alithibitisha mamlaka ya Papa juu ya Dola la Papa, na kuhakikisha siku za mbele uchaguzi wa Mapapa hautaingiliwa na serikali tena.[6] Wanahistoria wana wasiwasi kuhusu hati hiyo kuwa halisi.[7] Kwa vyovyote, baada ya Papa Paskali I kumtia taji la kifalme Lotari I, mwana wa Pius, mahusiano yalizidi kuharibika.

Papa Paskali I alipokea wamonaki wengi kutoka Dola la Roma Mashariki waliokimbia dhuluma ya serikali kuhusu picha takatifu[8], akawapa kazi ya kupamba makanisa aliyoyajenga au kuyakarabati[6][9] pamoja na kuwatetea kwa maandishi yake.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu[10][5], hasa tarehe 11 Februari[11][12] au 14 Mei[13][14].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Maandishi[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  3. Goodson, 2010, p. 9 & n.13.
  4.  One or more of the preceding sentences incorporates text from a publication now in the public domainKirsch, Johann Peter (1911). "Pope Paschal I". In Herbermann, Charles. Catholic Encyclopedia. 11. Robert Appleton Company. http://www.newadvent.org/cathen/11514a.htm.
  5. 5.0 5.1 O'Brien, Richard P. (2000). Lives of the Popes. New York: Harper Collins. pp. 132-133. ISBN 0-06-065304-3.  Unknown parameter |url-access= ignored (help)
  6. 6.0 6.1 John N.D. Kelly, Gran Dizionario Illustrato dei Papi, p. 271
  7. Claudio Rendina, I papi, p. 256
  8. Saint Paschal I | pope (en).
  9. Goodson, 2010, p. 3.
  10. CATHOLIC ENCYCLOPEDIA: Pope Paschal I.
  11. Martyrologium Romanum
  12. Zeno. Lexikoneintrag zu »Paschalis I, S. (2)«. Vollständiges Heiligen-Lexikon, Band 4. ... (de).
  13. 14.05: Memoria di San Pasquale I, Papa e Patriarca di Roma, che confessa la retta fede di fronte e contro l'eresia iconoclasta (verso l'anno 824). Jalada kutoka ya awali juu ya 2021-11-07. Iliwekwa mnamo 2022-04-15.
  14. "98. ПАСХАЛИЙ I", Церковно-Научный Центр "Православная Энциклопедия". (ru) 

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Goodson, Caroline J. 2010. The Rome of Pope Paschal I: Papal Power, Urban Renovation, Church Rebuilding and Relic Translation, 817–824. Cambridge University Press.
  • John N.D. Kelly, Gran Dizionario Illustrato dei Papi, Edizioni Piemme S.p.A., 1989, Casale Monferrato (AL), ISBN 88-384-1326-6
  • Claudio Rendina, I papi, Ed. Newton Compton, Roma, 1990

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Paskali I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.