Papa Nikolasi I

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Papa Nikolaus I)
Mt. Nikolasi I.

Papa Nikolasi I au Nikolasi Mkuu (takriban 82013 Novemba 867) alikuwa Papa kuanzia tarehe 24 Aprili 858 hadi kifo chake[1]. Alitokea Roma, Lazio, Italia[2].

Alimfuata Papa Benedikto III akafuatwa na Papa Adriano II.

Anakumbukwa kwa kuimarisha mamlaka ya Papa wa Roma, akichangia ustawi wa cheo hicho, hasa katika Ulaya Magharibi. Alisisitiza kuwa mamlaka hiyo iko juu ya watawala pia katika masuala ya imani na maadili.

Alikataa kutangaza ubatili wa ndoa ya mfalme Lothari II wa Lotharingia na mke wake, ingawa mfalme aliudai ili kumuoa Waldrada, mtaguso fulani uliukubali na jeshi la Wafaranki lilizingira Roma.

Mahusiano na Dola la Roma Mashariki yaliharibika kwa sababu aliunga mkono Patriarki Ignasi wa Konstantinopoli aliyekuwa ameondolewa madarakani ili kumpisha Fosyo.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 13 Novemba[3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Maandishi[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo=[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Nikolasi I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.