Nenda kwa yaliyomo

Papa Klementi I

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Klementi wa Roma)
Papa Klementi I. (taswira ya karne ya 15; Papa Klementi hakuvaa taji kama hili lililobuniwa miaka 1000 baadaye)

Papa Klementi I alikuwa Papa kuanzia takriban 92 hadi kifodini chake takriban 99[1]. Alitokea Roma, Italia.

Alimfuata Papa Anacletus akafuatwa na Papa Evaristus.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini na kutajwa katika Kanuni ya Kirumi.

Sikukuu yake ni tarehe 23 Novemba katika Ukristo wa magharibi[2] na tarehe 24 Novemba au 25 Novemba upande wa mashariki.

Maandishi

[hariri | hariri chanzo]

Maandishi pekee ambayo kwa hakika ni ya kwake ni waraka aliowaandikia Wakristo wa Korintho ili kuimarisha umoja na amani kati yao na kudhibiti uasi wao dhidi ya viongozi halali[3].

Kwa ajili hiyo Klementi anahesabiwa kuwa wa kwanza kati ya Mababu wa Kanisa waliofahamu Mitume wa Yesu[4]. Inawezekana ndiye aliyetajwa na Mtume Paulo katika Waraka kwa Wafilipi (4:3).

Sala yake

[hariri | hariri chanzo]

Wewe umefunua macho ya mioyo yetu, ili tukujue wewe Mungu pekee, uliye juu sana katika mbingu za juu, mtakatifu unayekaa kati ya watakatifu, ambaye unanyenyekeza ufidhuli wao wenye kiburi, unabatilisha mashauri ya mataifa, unawainua juu wanyonge na kuwashusha wanaojikweza, wewe ambaye unatajirisha na kufukarisha, unaua na kuhuisha, ambaye peke yako unafadhili roho na ni Mungu pekee wa kila mwenye mwili, unatazama vilindi, unachunguza matendo ya wanadamu, unawasaidia waliopo hatarini na ni mkombozi wa waliokata tamaa, ni muumbaji na mtunzaji wa roho zote, unazidisha mataifa duniani, ambaye kati ya wote umewachagua wanaokupenda, kwa njia ya Yesu Kristo Mwanao mpendwa, ambaye kwa njia yake umetulea, umetutakasa na kutuvika heshima.

Tunakusihi, Bwana, uwe kwetu msaidizi na tegemeo. Uwakomboe walio taabuni kati yetu, uwahurumie wanyonge, uwainue walioanguka, ujidhihirishe kwa wahitaji, uwaponye wagonjwa, uwarudishe waliojitenga na taifa lako, uwashibishe wenye njaa, uwafungue wafungwa wetu, uwaimarishe walio dhaifu, uwatulize walio duni.

Mataifa yote wapate kujua ya kuwa ndiwe Mungu, wewe peke yako, na ya kuwa Yesu Kristo ni Mwanao nasi tu wako wako na kondoo wa malisho yako.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Maandishi yake kwa Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]
  • Didakè yaani Mafundisho ya Mitume Kumi na Wawili na Waraka wa Mt. Klementi kwa Wakorinto, tafsiri ya B. Santopadre n.k. – ed. E.M.I. – Bologna (Italia) 1990 – ISBN 88-307-0321-4
  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
  3. "CATHOLIC ENCYCLOPEDIA: Pope St. Clement I". www.newadvent.org. Iliwekwa mnamo 2022-01-21.
  4. http://www.santiebeati.it/dettaglio/30150

Marejeo mengine

[hariri | hariri chanzo]
  • Clarke, W. K. Lowther, mhr. (1937). The First Epistle of Clement to the Corinthians. London: Society for the Promotion of Christian Knowledge.
  • Grant, Robert M., mhr. (1964). The Apostolic Fathers. New York: Nelson.
  • Loomis, Louise Ropes (1916). The Book of Popes (Liber Pontificalis). Merchantville, NJ: Evolution Publishing. ISBN|1-889758-86-8.
  • Lightfoot, J.B. (1890). The Apostolic Fathers. London: Macmillan.
  • Meeks, Wayne A. (1993). The origins of Christian morality : the first two centuries. New Haven: Yale Univ. Press. ISBN 978-0-300-05640-2.
  • Richardson, Cyril Charles (1943). Early Christian Fathers. The Library of Christian Classics. Philadelphia: Westminster Press.
  • Staniforth, Maxwell (1968). Early Christian writings. Baltimore: Penguin.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: