Nenda kwa yaliyomo

Papa Silverio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Silverius Mtakatifu)
Mt. Silveri.

Papa Silverio alikuwa Papa kuanzia tarehe 8 Juni 536 hadi mwaka 537[1]. Alitokea Frosinone, Italia[2].

Alimfuata Papa Agapeto I akafuatwa na Papa Vigilio.

Alizaliwa na Papa Hormisdas katika ndoa yake kabla ya kupata upadrisho.

Aliondoshwa madarakani mnamo mwezi Machi 537 kwa nguvu ya Theodora, mke wa Justiniani I, Kaisari wa Bizanti.

Huyo malkia alimpendelea shemasi Vigilio akitarajia ataunga mkono njama zake za kutetea uzushi wa Eutike.

Kumbe Silverio alikataa pia ombi la Theodora la kumrudisha madarakani Antimo kama Patriarki wa Konstantinopoli aliyekuwa ameondolewa na Papa Agapeto I kwa uzushi huohuo [3].

Basi, Silverio alifungwa na kupelekwa uhamishoni katika kisiwa cha Palmarola ambapo alijiuzulu tarehe 11 Novemba 537 akafariki kwa tabu nyingi na njaa tarehe 2 Desemba 537.

Angalau tangu karne ya 11 ameheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 2 Desemba[4].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • Duffy, Eamon (2006). Saints and Sinners: A History of the Popes. New Haven; London: Yale University Press. ISBN 978-0-30011-597-0.
  • Geary, Patrick J. (2002). The Myth of Nations: The Medieval Origins of Europe. Princeton, NJ: Princeton University Press. ISBN 978-0-69109-054-2.
  • McCabe, Joseph (1939). A History of the Popes. London: Watts & Co.
  • Procopius (1979). De Bello Gothico. Loeb Classical Library. Juz. la 3. Cambridge, MA: Harvard University Press.
  • Richards, Jeffrey (1979). The Popes and the Papacy in the Early Middle Ages, 476–752. London; Boston: Routledge and Kegan Paul. ASIN B01FIZI4RW.
  • Sanctoral.com. "Saint Silverius: Pope and Martyr". Lives of the Saints–Our Models and Protectors. Iliwekwa mnamo 21 Aprili 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • Sansilverioshrine.org. "History". San Silverio Shrine. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-01-31. Iliwekwa mnamo 21 Aprili 2019. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)

Marejeo mengine

[hariri | hariri chanzo]
  • Louise Ropes Loomis, The Book of Popes ("Liber Pontificalis"). Merchantville, NJ: Evolution Publishing. ISBN 1-889758-86-8 (Reprint of the 1916 edition. English translation with scholarly footnotes, and illustrations).

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Silverio kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.