Nenda kwa yaliyomo

Papa Damaso I

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Papa Damaso I.

Papa Damaso I (takriban 30411 Desemba 384) alikuwa Papa kuanzia tarehe 1 Oktoba 366 hadi kifo chake[1]. Alitokea Roma, Italia. Jina lake la kuzaliwa pia lilikuwa Damasus.

Alimfuata Papa Liberius akafuatwa na Papa Siricius.

Mchango wake mkubwa zaidi ni kuthibitisha kanuni ya Biblia kama ilivyo hadi leo katika Kanisa Katoliki.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni 11 Desemba.[2].

Athari yake katika suala la Deuterokanoni

[hariri | hariri chanzo]

Vitabu vya Deuterokanoni vilihesabiwa rasmi kuwa sehemu ya Biblia hasa kuanzia Hati ya Damasi au De explanatione fidei, iliyotolewa na Papa Damasus I mwaka 382 (kwa Kilatini).

Tafsiri ya Kilatini ya Hieronimo kilichoitwa Vulgata ilipata kuwa toleo muhimu katika Kanisa Katoliki hadi leo. Hieronimo mwenyewe alipotafsiri Biblia upya katika Kilatini alisema vitabu vya Septuaginta kama Kitabu cha Hekima, Kitabu cha Yoshua bin Sira, Kitabu cha Yudith na Kitabu cha Tobiti havistahili kuwemo katika Biblia lakini alivitafsiri ndani ya Vulgata kufuatana na maelekezo wa Papa Damaso I aliyemuagiza kazi.[3]

Orodha hiyo ya Papa Damaso I ilipata nguvu Afrika Kaskazini kutokana na Agostino wa Hippo kuifanya ipitishwe na Mtaguso wa Hippo (393), Mtaguso wa Tatu wa Kartago (397) na Mtaguso wa Nne wa Kartago (419).

Wakati huohuo Papa Inosenti I aliituma kwa askofu Exuperius wa Toulouse (405).

Baadaye Mtaguso wa Firenze (1442) na Mtaguso wa Trento (1546) ilivitambua rasmi kuwa sehemu za Biblia kamili kwa Kanisa Katoliki.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Maandishi yake

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.html/ index.html#holy-father
  2. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
  3. "Hic prologus Scripturarum quasi galeatum principium omnibus libris, quos de hebraeo vertimus in latinum, convenire potest, ut scire valeamus, quicquid extra hos est, inter apocrifa seponendum. Igitur Sapientia, quae vulgo Salomonis inscribitur, et Iesu filii Sirach liber et Iudith et Tobias et Pastor non sunt canone. Macchabeorum primum librum hebraicum repperi, secundus graecus est, quod et ex ipsa φράσιν probari potest." (Hieronimo katika "Prologus Galeatus" au utangulizi kwa vitabu vya Samueli na Wafalme katika Vulgata)
  • Chadwick, Henry. The Pelican History of the Church – 1: The Early Church.
  • Walker, Williston. A History of the Christian Church.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Damaso I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.