Nenda kwa yaliyomo

Hippo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Annaba, Algeria

Annaba (zamani: Hippo Regius, Kar.:عنابة anaba, Kifar. Bône) ni mji katika Algeria kwenye mwambao wa Mediteranea wenye wakazi 385,000 (2005).

Kuna chuo kikuu chenye wanafunzi 40,000.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mji ulianzishwa kwa jina la Hippo kama koloni la Wafinisia katika karne za KK.

Tangu mwaka 46 KK ulikuwa sehemu ya Dola la Roma.

Mkazi wake mashuhuri alikuwa Agostino Aurelio anayejulikana kama Agostino wa Hippo, askofu wa mji huo tangu mwaka 396 BK.

Agostino aliandika huko sehemu kubwa ya vitabu vyake.

Aliaga dunia wakati wa uvamizi wa Wavandali waliofanya Hippo kuwa mji mkuu wa ufalme wao Afrika kaskazini.[1]

Tangu mwaka 698 Hippo ilitekwa na Waarabu Waislamu waliouharibu wakaunda mji mpya kando ya maghofu ulioitwa "Beleb-El-Anab".

Jina hili likaendelea kubadilika kuwa "Annaba" wa mji wa leo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Bona, Algeria". World Digital Library. 1899. Iliwekwa mnamo 2013-09-25.