Papa Silvester I
Mandhari
(Elekezwa kutoka Papa Sylvester I)
Papa Silvester I alikuwa Papa kuanzia tarehe 31 Januari 314 hadi kifo chake tarehe 31 Desemba 335[1].
Alimfuata Papa Miltiades akafuatwa na Papa Marko.
Mtoto wa Rufinus, mkazi wa Roma, hatuna habari nyingi za maisha yake. Ila ni kwamba aliongoza Kanisa Katoliki kwa muda mrefu mara baada ya Kaisari Konstantino Mkuu kulipatia uhuru wa dini na kulijengea maabadi mengi, makubwa na mazuri.
Wakati wa utawala wake ulifanyika mtaguso mkuu wa kwanza (Nisea, leo nchini Uturuki, 325). Yeye hakuhudhuria, ila alituma wajumbe wawili akathibitisha maamuzi yaliyofikiwa.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Mapapa
- Mababu wa Kanisa
Maandishi yake
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.html
- ↑ Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- H.U. Instinsky: Silvester I. In: Josef Höfer, Karl Rahner (Hrsg.): Lexikon für Theologie und Kirche. 2. Auflage. Band 9. Herder, Freiburg im Breisgau 1964, Sp 757–758.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- Kuhusu Papa Silvester I katika Kamusi Elezo ya Kikatoliki
- Maisha yake Archived 5 Machi 2016 at the Wayback Machine.
- Colonnade Statue in St Peter's Square
- Legenda Aurea
- Akathist to Saint Sylvester
- Canon to Saint Sylvester
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Silvester I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |