Papa Benedikto XVI

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
StPetersBasilicaEarlyMorning.jpg
Imani

Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Dhambi Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria


Muundo

Papa: Benedikto XVI
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki

Historia

Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi

Ibada

Liturujia Mwaka wa Kanisa
Ekaristi Liturujia ya Vipindi

Mapokeo ya liturujia

Liturujia ya Kilatini (Roma Milano Toledo Braga Lyon)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Ugiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia

Papa Benedikto XVI

Papa Benedikto XVI (amezaliwa 16 Aprili 1927; jina la Kilatini: Benedictus XVI; kwa Kiitalia: Benedetto XVI) ni papa tangu 19 Aprili, 2005 baada ya kifo cha Papa Yohane Paulo II.

Ni mwandamizi wa 264 wa Mtume Petro na Papa wa kwanza kutoka Ujerumani baada ya miaka 1000 hivi.

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Joseph Alois Ratzinger.

Alipadirishwa tarehe 29 Juni 1951 pamoja na kaka yake Georg.

Baada ya kupata udaktari katika teolojia na kufundisha miaka kadhaa, alishiriki kama mtaalamu katika Mtaguso Mkuu wa Vatikano II.

Tarehe 24 Machi 1977 alichaguliwa na Papa Paulo VI kuwa Askofu mkuu wa Munchen na Frisingen akapewa daraja hiyo tarehe 28 Mei mwaka huohuo.

Tarehe 27 Juni mwaka huohuo Paulo VI alimteua pia kardinali na kutokana na cheo hicho alishiriki uchaguzi wa Papa Yohane Paulo I na Yohane Paulo II mwaka 1978.

Tarehe 25 Novemba 1981 Yohane Paulo II alimteua kuwa mkuu wa Idara ya Mafundisho ya Imani. Hivyo tarehe 15 Februari 1982 aliacha uongozi wa jimbo kuu akashika kazi hiyo mpya mpaka alipochaguliwa Papa.

Katika kazi hiyo aliandaa Katekisimu ya Kanisa Katoliki tangu 1986 hadi 1992) na Ufupisho Makini wa katekisimu hiyo tangu 2003 hadi 2005).

Baada ya kuchaguliwa Papa aliendeleza juhudi za mtangulizi wake katika utekelezaji wa Mtaguso.

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine