Papa
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Papa ni cheo cha kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kote. Cheo hiki kinaenda sambamba na askofu wa Roma. Kuna orodha ya mapapa.
Yaliyomo |
[hariri] Asili ya cheo cha Papa
Kiasili neno la Kiitalia "Papa" lamaanisha "Baba", nalo likawa cheo kwa nia ya kumtaja askofu wa Roma kwa heshima ya pekee. Msingi wa heshima hii ni imani ya kuwa askofu wa Roma ni mwandamizi wa Petro mtume wa Yesu. Wakatoliki huamini ya kwamba Petro alipewa na Yesu kazi ya kuongoza kanisa kwa niaba yake na ya kwamba jukumu hilo linaendelea kati ya waandamizi wa Petro kwenye kiti cha askofu wa Roma.
[hariri] Majina ya mapapa
Papa huchaguliwa na makardinali wa kanisa katoliki baada ya mtangulizi wake kufa au kujiuzulu. Baada ya kuchaguliwa papa mpya anaweza akapata jina jipya. Tangu 2005 ni Papa Benedikto XVI, ambaye awali aliitwa Joseph Ratzinger.
Majina ya mapapa wengine wa kanisa katoliki yapatikana katika orodha ya mapapa.
[hariri] Mkuu wa Vatikano
Papa ni pia mkuu wa nchi ya Mji wa Vatikano iliyopo ndani ya mji wa Roma (Italia).
[hariri] Cheo cha "Papa" penginepo
Cheo cha Papa hutumiwa pia na baadhi ya madhehebu mengine ya Kikristo kwa viongozi wao hasa kwa mkuu wa Kanisa la Kikopti huko Misri.
| Makala hiyo kuhusu "Papa" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Papa kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |

