Teolojia

Kutoka Wikipedia

Neno hilo linatokana na maneno mawili ya Kigiriki: θέος, theos, "Mungu", + λογία, logia, "usemi"). Hivyo maana yake ni Elimu juu ya Mungu. Hiyo haitenganiki na utendaji wake wa nje, yaani uhusiano wake na viumbe vyote.

Jina lingine la fani hiyo lenye asili ya Kiarabu ni Tauhidi. Hilo linatumiwa zaidi na Waislamu.

Kumbe ikitajwa kwa jina la mkopo kutoka Kigiriki, fani hiyo inachunguza hasa imani ya Kikristo kadiri ya Ufunuo wa Mungu uliokamilika katika Yesu Kristo na Mitume wake.

Kwa sababu hiyo inategemea hasa Maandiko Matakatifu ya Biblia, lakini pia, kadiri ya madhehebu husika, Mapokeo ya Mitume yasiyoandikwa na mamlaka hai ya Kanisa (Ualimu).

Vifaa binafsi