Papa (samaki)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Papa
Papa (Australia) (Carcharhinus amblyrhynchos)
Papa (Australia) (Carcharhinus amblyrhynchos)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Chondrichthyes (Samaki wenye gegedu)
Nusungeli: Elasmobranchii (Papa na taa)
Oda ya juu: Selachimorpha (Papa)
Ngazi za chini

Carcharhiniformes (Papa-chini)
Heterodontiformes (Papa Kichwa-ng'ombe)
Hexanchiformes (Papa Matamvua-sita)
Lamniformes (Papa-nguru)
Orectolobiformes (Papa Madoadoa)
Pristiophoriformes (Papa-msumeno)
Squaliformes (Papa-mbwa)
Squatiniformes (Papa Bapa)

Meno ya papa katika makumbusho mjini Baltimore

Papa ni kundi la spishi 500 za samaki wenye kiunzi cha gegedu badala ya mifupa. Gegedu ni dutu ya kunyambuliwa kama mpira mgumu lakini laini kuliko mifupa kamili. Karibu spishi zote za papa wanaishi katika maji ya chumvi baharini.

Papa wengi ni wavindaji wanaokula samaki na wanyama wengine wa baharini. Spishi kadhaa wanahofiwa kwa sababu kushika wanadamu. Lakini papa wakubwa sana hula planktoni kama nyangumi wakubwa.

Papa mkubwa kabisa ni papa nyangumi (Rhincodon typus) anayefikia urefu wa mita 14 na uzito wa tani 12 ambaye ni pia samaki mkubwa kabisa duniani na hula planktoni. Spishi ndogo kabisa ni Etmopterus perryi, wenye urefu wa sentimita 21 tu.

Spishi nyingi za papa ziko hatarini ya kupotea kwa sababu wanavuliwa mno.

Papa huwa na meno mengi yanayoendelea kukua muda wote wa maisha yake mstari baada ya mstari wa meno yanayoanza kukua nyuma ya meno ya nje na kuchukua nafasi yao mfululizo.

Wana uwezo mkubwa wa kunusa ndani ya maji hasa damu ya kiumbe aliyeumizwa kwenye umbali wa kilomita. Kupitia ngozi wanatambua pia mwendo ndani ya maji na wanaelekea penye chanzo cha mwendo.

Spishi nne wametambuliwa kuwa ni hatari kwa wanadamu. Lakini jumla ya ajali ambako mwanadamu anang'atwa na papa ni takriban 100 kwa mwaka kote duniani; mara nyingi watu wanajeruhiwa na mwaka 2007 kuna ya kifo kimoja kutokana na papa. Wataalamu wanajadiliana kama papa wanashambulia kweli au kama wanajisikia mara nyingi wameshambuliwa na watu wanaowakaribia mno au kama papa anamchanganya mwanadamu na windo la kawaida.

Kinyume chake kuna papa milioni 200 wanaouawa kila mwaka na wanadamu.

Spishi za Afrika ya Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa (samaki) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Wikimedia Commons ina media kuhusu: