Nyangumi
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Nyangumi | ||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||
|
Nyangumi ni wanyama wa bahari ambao ni mamalia. Wananyonyesha wadogo wao si samaki. Pamoja na nguva ni mamalia wa pekee wanaoishi kwenye maji tu. Ni oda ya wanyama yenye spishi 80 karibu wote wako baharini isipokuwa kuna spishi chache za pomboo wanaokaa kwenye maji matamu ya mito mikubwa kama Ganges au Amazonas. Jina la kisayansi la oda ni Cetacea.
Mwili wote unalingana na maisha ya majini. Nyangumi wanaotupwa kwenye nchi kavu wanakufa haraka; wanakauka, uzito wa mwili unagandamiza mapavu kwa sababu wanakosa ueleaji wa maji.
Hata hivyo muundo wa mwili bado ni sawa kama mamalia wengine:
- wanapumua kwa kutumia mapafu; kutegemeana na spishi zinaweza kuzama na kukaa chini ya maji kuanzia dakika kadhaa hadi masaa mawili.
- Huwa na moyo yenye vyumba viwili inayoweza kusambaza oksijeni mwilini kote.
- Nyangumi huwa na damu moto yaani wanaweza kutunza halijoto ya wastani mwilini tofauti na samaki wanaobadilika halijoto ya mwili kulingana na halijoto ya mazingira.
- Wanazaa watoto waliokamilika tayari na kuwanyonyesha maziwa yenye mafuta mengi kwa kutumia viwele vyao. Kiinitete hukua mwilini hadi kuwa mnyama kamili jinsi ilivyo na mamalia wengi.
Spishi nyingi za nyangumi ni kubwa sana. Nyangumi anayitwa buluu (Balaenoptera musculus, Kiing. Blue Whale) anaweza kufikia uzito wa tani 200 na urefu wa mita 33. Nyangumi wadogo ni hasa familia ya pomboo ambao wadogo wanafikia urefu wa mita na nusu pekee.
Mara nyingi spishi za nyangumi zinatofautishwa kutokana na meno yao:
- wale wanaovinda samaki au wanayama wakubwa wengine wa bahari wana meno ya kawaida.
- wale wanaokula planktoni (viumbe vidogo sana baharini) hawana meno bali mifupa ya kinywani ambao si mifupa ya kweli inaundwa na kitu kinachofanana na kucha za vidole. Mifupa hii inakaa kama meno ya chanuo inafanya kazi ya filta; nyangumi huyi anafungua mdomo na kujaza nafasi maji pamoja na yote yaliyomo kama uduvi wadogo sana; ulimi unasukuma maji kupitia chanua ya mifupa ya kinywani na windo unabaki ndani kama chakula.
[hariri] Viungo vya Nje
- ARKive - images and movies of Whales, Dolphins and Porpoises
- American Cetacean Society
- British Cetacean Site especially interesting is taxonomy
- Cetacea.org homepage
- Walker's Mammals of the World Online - Cetaceans
- Tursiops.org: Current Cetacean-related news
- Whales, Dolphins, Porpoises and Cetaceans Forum
| Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nyangumi kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |