Nyama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyama ya wanyama kadhaa.

Nyama ni sehemu za mwili wa wanyama zinazoliwa kama chakula au kitoweo.

Kwa watu wengi nyama ni chakula muhimu kwa sababu ina protini nyingi ndani yake pamoja na mafuta. Nyama huliwa baada ya kuipika, kuchoma au kukaanga. Kuna sehemu za dunia ambako watu wamezoea kula nyama mbichi wakiteua sehemu lainilaini, kwa mfano nyama ya kusagwa au maini.

Uchumi wa nyama[hariri | hariri chanzo]

Moja ya bucha ya nyama huko Algeria

Gharama ya nyama ni kubwa kushinda chakula cha mboga kwa sababu kiuchumi nyama ni mboga iliyobadilishwa umbo. Njia yake ni wanyama kula majani na majani haya yakikuza mnyama huwa nyama baada ya kuchinjwa. Kwa njia hiyo kilogramu moja ya protini ya nyama huhitaji kilogramu 5 hadi 10 za protini ya mboga kama lishe ya wanyama. Kwa lugha nyingine ekari zinazolisha wanyama wa kushibisha watu 100 zinaweza kulisha watu 500 hadi 1,000 kwa njia ya nafaka, maharagwe n.k.

Katika mazingira asilia hili si tatizo kubwa kwa sababu maeneo yabisi hayakufaa kwa kilimo lakini wafugaji wa kuhamahama waliweza kuzunguka huko na wanyama wao ilhali nchi yenye mvua na rutuba ilitumiwa kwa kilimo cha mimea ya kulisha watu.

Kilimo cha kisasa kimebadilisha muundo huo kwa sababu sehemu kubwa ya mavuno hutumiwa kwa lishe ya wanyama. Tatizo lake linaonekana pale ambako nchi tajiri kama Marekani au zile za Ulaya zinanunua nafaka au maharagwe kote duniani kama lishe ya wanyama wao. Kwa njia hiyo wanasababisha bei ya vyakula hivi kupanda hata wakazi maskini wanaona bei ya vyakula zinapanda kushinda uwezo wao.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Uthibitisho wa Paleontolojia unaonyesha kuwa nyama ilikuwa sehemu kubwa ya chakula cha binadamu toka kale. Jamii za kale za wawindaji zilipata nyama kwa kuwinda wanyama wakubwa kama [kulungu]]

Wanyama ambao sasa ni vyanzo vikuu vya nyama walianza kuliwa toka mwanzo wa maendeleo ya ustaarabu:

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyama kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.