Karne ya 19
Lango la Historia | Lango la Biografia | Karibuni | Orodha ya Miaka
◄ | Karne ya 17 | Karne ya 18 | Karne ya 19 | Karne ya 20 | Karne ya 21
Miaka ya 1800 | Miaka ya 1810 | Miaka ya 1820 | Miaka ya 1830 | Miaka ya 1840 | Miaka ya 1850 | Miaka ya 1860 | Miaka ya 1870 | Miaka ya 1880 | Miaka ya 1890
Karne ya 19 ilikuwa kipindi cha miaka mia moja kati ya 1800 na 1900. Kikamilifu kilianza tarehe 1 Januari 1801 na kuishia 31 Desemba 1900.
Kama kila "karne" ni kipindi kinachohesabiwa kwa hiari ya binadamu kwa sababu ni mgawanyo wa kalenda tu - hali halisi, maendeleo na mabadiliko makubwa hayafuati migawanyo ya kalenda ya kibinadamu.
Hata hivyo kipindi hiki cha karne ya 19 kilikuwa kipindi muhimu sana katika historia ya binadamu.
[hariri] Watu na matukio
| Karne: Karne ya 18 | Karne ya 19 | Karne ya 20 |
| Miongo na miaka |
| Miaka ya 1800 | 1800 1801 1802 1803 1804 1805 1806 1807 1808 1809 |
| Miaka ya 1810 | 1810 1811 1812 1813 1814 1815 1816 1817 1818 1819 |
| Miaka ya 1820 | 1820 1821 1822 1823 1824 1825 1826 1827 1828 1829 |
| Miaka ya 1830 | 1830 1831 1832 1833 1834 1835 1836 1837 1838 1839 |
| Miaka ya 1840 | 1840 1841 1842 1843 1844 1845 1846 1847 1848 1849 |
| Miaka ya 1850 | 1850 1851 1852 1853 1854 1855 1856 1857 1858 1859 |
| Miaka ya 1860 | 1860 1861 1862 1863 1864 1865 1866 1867 1868 1869 |
| Miaka ya 1870 | 1870 1871 1872 1873 1874 1875 1876 1877 1878 1879 |
| Miaka ya 1880 | 1880 1881 1882 1883 1884 1885 1886 1887 1888 1889 |
| Miaka ya 1890 | 1890 1891 1892 1893 1894 1895 1896 1897 1898 1899 |
Mabadiliko mengi yalianzia Ulaya na kuenea duniani, hivyo karne hii imeitwa na wataalamu "karne ya Ulaya".
Baadhi ya tabia za pekee za karne hii ni kama zifuatazo:
- Mapinduzi ya viwandani: yaliwahi kuota mizizi katika Uingereza kabla ya 1800, lakini katika karne hii yalienea katika nchi za Ulaya na kuzitofautisha kwa uwezo wao
- Nchi zilizopita katika mapinduzi ya viwandani ziliongezeka nguvu za kiuchumi na kijeshi kushinda mataifa nje ya mapinduzi haya
- Mtindo wa ubepari ulipata umuhimu na kugusa maisha ya watu wengi
- Tabaka jipya la wanafanyakazi lilijitokeza
- Tabaka la makabaila lilipungukiwa umuhimu wake katika jamii za nchi zilizoshiriki katika mapinduzi ya viwandani
- Maisha ya viwandani na maisha ya mjini yalivunja nguvu ya maisha ya mashambani hivyo mapokeo na desturi nyingi zilizowahi kuendelea tangu karne nyingi
- matunda ya fikra za mwangaza yalisababisha
- kutokea kwa sayansi ya kisasa
- ukosoaji wa dini
- Idadi ya watu duniani ilianza kukua haraka kushinda miaka yote ya historia ya awali kwa sababu ya
- matokeo ya teknolojia na sayansi yaliongeza kiasi cha chakula kilichopatikana kwa watu
- sayansi ya tiba iligundua njia za kupambana na magonjwa
- Nchi kadhaa za Ulaya zilitumia nguvu mpya ya kueneza utawala wao nje ya Ulaya
- Ukoloni ulienea : mwanzoni mwa karne hii polepole, mwishoni kwa mbio
- Fundisho jipya la "utaifa" lilianza kubomoa misingi ya madola makubwa ya kimataifa katika Ulaya kama Uturuki, Austria, Urusi.
- Katika siasa madola kadhaa yaliyowahi kuratibu maisha ya watu tangu karne nyingi yalipungukiwa, kuvunjwa au kupotea kabisa kama vile:
- Dola takatifu la Kiroma la Ujerumani katika Ulaya ya Kati
- Dola la Moghul katika Bara Hindi
- Dola la Uturuki (Uturuki, Afrika ya Kaskazini, Asia ya Magharibi)
- Dola la Hispania (Hispania, Amerika ya Kusini na Ufilipino)
- Dola la Uingereza lilitokea kuwa dola kubwa duniani
- Utumwa ulipungua sana duniani
- Ukristo ulienea upya nje ya Ulaya kwa njia ya misheni ya kisasa baada ya kurudishwa nyuma na Uislamu tangu karne ya 7
- Huko Manchester ilianzishwa International Football Association Board, iliyoratibu sheria za kandanda (1882)
- Mfereji wa Suez unatenganisha Afrika na Asia
- Uhamiaji wa umati wa watu katika nchi nyingine
- Mwanzo wa ujamaa na ukomunisti
- Papa Pius IX na Mtaguso wa kwanza wa Vatikano
- Ludwig van Beethoven, Frédéric Chopin, Richard Wagner e Franz Liszt, wanamuziki
- Louis Pasteur, mwanasayansi
- Guglielmo Marconi, aliyebuni redio
- Malkia Viktoria wa Uingereza
- Otto von Bismarck, Kansela wa UJerumani
- Ndugu Lumière, waliobuni sinema
- Abraham Lincoln, rais wa Marekani aliyefuta utumwa nchini
- Charles Darwin (1809 - 1882), Mwingereza mwanasayansi
- George Stephenson aliyebuni treni
- Thomas Alva Edison aliyebuni taa na santuri
- Inabuniwa mota ya umeme
- Edward Jenner aliyebuni chanjo
- Inaanza kutengenezwa Coca-Cola
- Inaanza kutengenezwa aspirini
- Antonio Meucci aliyebuni simu
- Inabuniwa pikipiki
- Linabuniwa gari