Utumwa
Utumwa ni mfumo unaotoa fursa kwa binadamu kummiliki binadamu mwenzake kama mali yake. Binadamu anayemilikiwa anakuwa na hadhi sawa na chombo au kifaa chochote kinachoweza kuuzwa.
Mfumo huu ulikuwa maarufu kabla ya harakati za ukoloni duniani mathalani karne ya 15 ambapo watumwa walihitajika katika shughuli za kilimo na uchimbaji madini katika sehemu mbalimbali za ulimwengu.
Mfumo huu uunda matabaka ya "mabwana" ambao humiliki watumwa na "watwana" ambao ni watumwa wenyewe.
[hariri] Utumwa tofautitofauti
Katika historia zilitokea aina mbalimbali za utumwa.
Kulikuwa na utumwa wa muda (yaani mtu huwa mtumwa kwa miaka kadhaa) au kwa maisha yote. Kulikuwa na utaratibu ambako watoto wa mtumwa walikuwa watumwa tena hivyo kuzaliwa watumwa; kulikuwa pia na utaratibu ya kwamba watoto wa watumwa waliazamiwa kama watu huru.
Kulikuwa na jamii ambako watumwa hawakuwa na haki kabisa yaani mabwana waliweza kuwatendea jinsi walivyotaka hata kuwaua lakini kulikuwa pia na jamii zilizojua haki fulani za watumwa; watumwa waliweza kuwa na mali ya binafsi na kwa njia hii hata kununua uhuru wao kutoka kwa mabwana.
Watumwa katika utumishi wa watawala waliweza kupata nafasi muhimu katika jamii; mfano ni wamameluki wa Misri waliokuwa watumwa wanajeshi wakatawala nchi hii kwa karne kadhaa.
[hariri] Chanzo cha utumwa
Chanzo cha utumwa kilikuwa mara nyingi ama vita ama madeni. Vitani wafungwa wakauzwa kama watumwa wakihesabiwa kama sehemu ya uwindo wa washindi. Sababu kuu nyingine ilikuwa madeni ya watu waliokamatwa na kuuzwa ili madeni yalipiwe kwa njia hii.
Mahitaji wa kiuchumi kwa watumwa wengi yalisababisha biashara ya watumwa.