Asilimia
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Asilimia ni njia ya kutaja uhusiano kati ya viasi viwili. Alama yake ni %. Kiasi kimoja huteuliwa kuwa ni namba ya 100 ya kiasi kingine. Sehemu yake ya mia ni 1 %.
Sasa inawezekana kugawa kiasi kingine kwa ile 1% na kuona inashika asilimia ngapi za kiasi husianifu.
[hariri] Mfano
Mfano: Jumla ya maksi kwenye mtihani ni 250. Sheria inasema ya kwamba 65 % ni sharti kwa kupita. Je maksi ngapi zinahitajika ila kupita mtihani huu?
Jibu: Jumla ni 250 hivyo 250 zachukuliwa kama asilimia mia moja. Sehemu ya mia moja yaani 1 % ni 2.5. Asilimia 65 ni 2.5 zidisha 65 jumla 162.5. Maana yake kuanzia maksi zisizopungua 163 mwanafunzi amepita.
[hariri] Sehemu na asilimia
Kuna viwango kadhaa za sehemu zinazokumbukwa kirahisi kwa asilimia:
| Sehemu | Asilimia |
|---|---|
| Nusu | 50 % |
| robo | 25 % |
| robo tatu | 75 % |
| theluthi | 33 % |
| humusi | 20 % |
| humusi mbili | 40 % |
| ya kumi | 10 % |
Sehemu kama sudusi haifai vizuri kwa sababu asilimia yake ni 16.66 %.
| Makala hiyo kuhusu "Asilimia" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Asilimia kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |