Pesa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Pesa za Afrika ya Mashariki
Pesa ya Euro

Pesa ni chombo cha kubadilishana bidhaa na huduma kati ya watu. Pesa yenyewe haina faida haitoshelezi mahitaji ya kibinadamu ila imekubaliwa katika jamii kama njia ya kujipatia mahitaji mengine.

Kuna maneno mengine kwa pesa kama vile hela, fedha au sarafu.

Yaliyomo

[hariri] Historia ya pesa

Kiasili watu walibadilishana vitu kwa mfano ng'ombe mmoja kwa mbuzi kadhaa au mazao kwa samaki nk. Baadaye imeonekana ya kwamba itasaidia zaidi kama kiwango fulani inapatikana kwa vitu vyote.

Metali zilizokuwa haba zilitumiwa kama kipimo hiki kwa mfano dhahabu, fedha au shaba. Vilipimwa kufuatana uzito. Hatua iliyofuata ilikuwa kutumia vipande vya metali hizi vilivyogongwa mihuri halafu hapakuwa na lazima ya kuvipima kimoja-kimoja. Inavyojulikana Wachina walikuwa watu wa kwanza waliochukua hatua hii katika milenia ya 2 KK. Hii ilikuwa mwanzo wa sarafu.

Pesa hutolewa na serikali ya nchi au na taasisi kama benki kuu inayofanya kazi hii kwa niaba ya serikali. Mwanzoni sarafu ilikuwa sawa na kiasi fulani cha dhahabu au fedha.

Hatua nyingine ilikuwa kutolewa kwa pesa ya karatasi au benknoti zilizoahidi kumpatia mtu yeyote kiasi kilichoandikwa kwa dhahabu au fedha yenyewe. Kwa muda mrefu benki kuu zilikuwa na hazina ya dhahabu iliyolingana na kiasi cha benknoti zilizochapishwa. Tangu mwisho wa karne ya 20 nchi kadhaa zilianza kutoa benknoti za plastiki kwa sababu zinadumu kushinda noti za karatasi tena ni vigumu zaidi kutengeneza pesa bandia.

Katika karne ya 20 nchi zote zilifanya hatua ya kuacha makadirio ya dhahabu kwa sababu thamani ya bidhaa katika jamii ilipita kiasi cha dhahabu iliyopatikana. Siku hizi jumla ya pesa inayotolewa inatakiwa kulingana na thamani ya rasilmali ya taifa fulani.

Pale ambako serikali inachapisha benknoti kushinda kiwango hicho thamani ya pesa inashuka na mfumko wa bei inatokea.

Pesa 1 ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (hadi 1904) - nyuma; maandishi yasema: "Deutsch-Ostafrikanische Gesellschaft 1892"
Pesa 1 ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (hadi 1904) - mbele; maandishi yasema: "sharaka almaniya 1309"

[hariri] "Pesa" ya Kihindi kama sarufi

Asili ya neno "pesa" katia lugha ya Kiswahili ni sarufi ndogo ya Kihindi iliyokuwa kitengo cha rupia. Rupia 1 ilikuwa na pesa 64 ikawa sarufi ya kawaida katika Afrika ya Mashariki kabla ya kipindi cha ukoloni.

[hariri] "Pesa" ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani

Wajerumani walipoanzisha koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani waliendelea kutoa sarufi kwa jina la rupia na pesa hadi 1904. Pesa 64 zilifanya rupie 1. Mwaka 1904 walibadilisha muundo na sarufi ya pesa ilipotea badala yake heller ilianzishwa. Lakini neno lilibaki katika lugha.

Sarufi za pesa zilitolewa na Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki. Zilikuwa na maandishi ya Kiarabu upande moja na maandishi ya Kijerumani nyuma yake. Upande wa Kiarabu ilionyesha mwaka wa kutolewa kama tarehe baada ya hijra na upande wa Kijerumani ulionyesha mwaka BK. Maandishi yalikuwa jina la kampuni tu kwa Kiarabu na Kijerumani; upande wa Kijerumani ulikuwa na tai mwenye taji kama nembo la Dola la Ujerumani.

[hariri] Viungo vya Nje

  • Linguistic and Commodity Exchanges by Elmer G. Wiens. Examines the structural differences between barter and monetary commodity exchanges and oral and written linguistic exchanges.
ThreeCoins.svg Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pesa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine