Ng'ombe
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Ng'ombe | ||||||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kundi la ng'ombe
|
||||||||||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
|
Ng'ombe ni wanyama wakubwa wa jenasi Bos. Spishi ya ng'ombe ina nususpishi au aina nyingi lakini ni spishi moja tu.
Ng'ombe hula manyasi na kutembea kwa vidole viwili.
Asili yake ni aina za ng'ombe wa pori waliofugwa kwa sababu ya nyama na maziwa. Katika nchi nyingi anatumiwa pia kama mnyama wa mizigo anayevuta plau au magari.
Wataalamu huamini ya kwamba aina zote za ng'ombe zina asili katika mashariki ya kati mnamo milenia ya 9 KK ambako watu waliwahi kuwafuga nas kutoka hapa ufugaji ng'ombe ulisambaa kote duniani.
Ng'ombe wanapatikana kote duniani na kuna aina kwa kila namna ya hali ya hewa. Wengine huishi katika milima baridi za Uskoti au Skandinavia, wengine katika joto la Afrika au Australia.
Wanacheua chakula chao na huwa na tumbo lenye vyumba vinne. Baada ya kula nyasi mara ya kwanza wanirudisha kutoka chumba cha kwanza cha tumbo na kuitafuna tena. KWa njia hii wanapata lishe nyingi kutoka nyasi.
|
Mchezo wa ng'ombe uanpendwa katika nchi zeye utamaduni wa Kihispania |
[hariri] Viungo vya Nje
- Cattle Breeds website - Oklahoma State University
- PBS Nature: Holy Cow (about cows in general)