Australia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Commonwealth of Australia
Jumuiya ya Australia
Bendera ya Australia Nembo ya Australia
Bendera Nembo
Wito la taifa: (hakuna)
Wimbo wa taifa: Advance Australia Fair
Wimbo la kifalme: God Save the Queen
Lokeshen ya Australia
Mji mkuu Canberra
35°15′ S 149°28′ E
Mji mkubwa nchini Sydney
Lugha rasmi Kiingereza (hali halisi, si kisheria)1
Serikali
1: Malkia wa Australia,
2: Gavana Mkuu,
3: Waziri Mkuu
Shirikisho la kifalme
1: Elizabeth II wa Uingereza,
2: Michael Jeffery,
3: Julia Gillard
Uhuru
Katiba ya Australia
1.1. 1901
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
7,741,220 km² (ya 6)
1
Idadi ya watu
 - 2006 kadirio
 - 2001 sensa
 - Msongamano wa watu
 
20,555,300 (53rd)
18,972,350
2.6/km² (224th)
Fedha Australian dollar (AUD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
various2 (UTC+8–+10)
various2 (UTC+8–+11)
Intaneti TLD .au
Kodi ya simu +61
1English does not have de jure official status (source)
2There are some minor variations from these three time zones, see Time in AustraliaAustralia ni bara pia ni nchi. Ni bara ndogo kuliko zote duniani, na pia ni kisiwa kikubwa kuliko zote. Iko kusini ya Indonesia na magharibi ya New Zealand. Ikiwa na eneo la 7.682.300 km² ni bara ndogo kabisa duniani, kama nchi ni nchi kubwa ya sita. Mara nyingi visiwa vya New Zealand huhesabiwa kuwa sehemu ya bara la Australia. Vilevile Australia huangaliwa pamoja na visiwa vya Pasifiki katika orodha la mabara ya dunia kama "Australia na Pasifiki".

Idadi ya wakazi ni milioni 20 (mwaka 2004).

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Climatic zones in Australia, based on Köppen classification

Bara la Australia linakaa juu ya bamba la Australia likiwa na eneo la 7,617,930 km². Umbali kati ya magharibi na mashariki ni 4,000 km na kati ya kaskazini na kusini umbali ni 3,700 km. Kwa jumla ina pwani lenye urefu wa kilomita 34,218. Australia huzungukwa na bahari ya Hindi, bahari ya Pasifiki na Bahari ya Kusini.

Bara linakaa kwenye sehemu imara ya bamba la Australia bila mipaka ya gandunia na kwa hiyo hakuna volkeno; matetemeko ya ardhi ni madogo tu.

Great Barrier Reef mbele ya pwani la mashariki-kaskazini ni vipwa vya matumbawe vikubwa duniani ina urefu wa kilomita 2,000.

Sehemu kubwa ya bara ni jangwa au maeneo yabisi sana. Takriban asilimia 40 ya eneo limefunikwa na matuta ya mchanga. Ardhi yenye rutba iko kusini-mashariki na kona ya kusini-magharibi pamoja na hali ya hewa isiyo na joto kali. Hali ya hewa kwenye kaskazini ni kitropiki na hapa kuna misitu minene pamoja na savana na jangwa.

Sehemu kubwa ya uso wa nchi ni tambarare na majangwa. Kwenye pwani la mashariki na pia upande wa magharbi kuna safu za milima inayopanda hadi kimo cha mita 2,200. Sehemu ya juu kabisa huitwa milima ya theluji au Alpi za Australia na mlima wa Mount Kosciuszko unafikia kimo cha mita 2,229. Hapa kuna barafuto za kudumu.

Sehemu ya duni iko kwenye beseni ya ziwa Eyre iliyopo mita 17 chini ya uwiano wa bahari. Tako za beseni hii mata nyingi ni kavu kabisa panajaa mara chache tu baada ya mvua mkubwa sana.

Mahali pakavu kabisa ni jangwa la Simpson lenye usimbishaji chini ya 200 mm kwa mwaka.

Sehemu kubwa ya bara haina watu. Wakazi wengi pamoja na miji yote wako kwenye pwani la mashariki na kusini. Uchumi katika maeneo yabisi ni hasa ufugaji wa kondoo milioni 130 na ng'ombe milioni 25.

Miji mikubwa ni Sydney (wakazi mio 3.7), Melbourne (wakazi mio 3.6), Brisbane (wakazi mio 1.7), Perth (wakazi mio 1.4) na Adelaide (wakazi mio 1.1).

Mji mkuu Canberra (wakazi mio 308,700) ilijengwa kati ya Sydney na Melbourne kwa sababu miji hii miwili ilishindwa kukubaliana kati yao ni mji upi unaostahili kuwa mji mkuu.

Mito muhimu inaanza katika Alpi za Australia ni Murray na Darling inayomwagilia beseni ya Murray-Darling na hii ni eneo muhimu la kilimo cha Australia. Mingine ni Mto Snowy na Mto Murrumbidgee, halafu mto Fitzroy (Queensland), mto Ord, mto Swan (Australia ya Magharibi), mto Derwent, mto Tamar (Tasmania) na mto Hawkesbury (New South Wales).

Ekolojia[hariri | hariri chanzo]

Australia ilitengwa na mabara mengine miaka milioni mingi iliyopita. Kwa sababu hiyo kuna aina nyingi za pekee za mimea na wanyama zisizopatikana penginepo duniani. Wanyama wa pekee ni kwa mfano kanguru na koala. Miti ya Australia kama vile mkalitusi imepelekwa kote duniani katika nchi zenye hali ya hewa ya kufaa.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Watu wa kwanza walifika Australia takriban miaka 50,000 iliyopita. Walitunza utamaduni wa wavindaji-wakusanyaji hadi kufika kwa ukoloni.

Hakuna habari kama watu wa Asia walifikia Australia lakini tangu karne ya 17 BK Waholanzi halafu Waingereza walifika kwa jahazi zao.

Australia ikawa mahali pa koloni ya kigereza na wafungwa kutoka Uingereza walipelekwa hapa katika karne ya 19 BK. Baadaye walifika pia walowezi huru.

Idadi ya Waustralia asilia imepungua sana kutokana na magonjwa mapya wakiambukizwa na Wazungu pia wametendewa vibaya na kufukuzwa katika sehemu kubwa ya nchi yao.

Australia ilipata uhuru wake mwaka 1901 lakini inaendelea kumkubali malkia ya Uingereza kama Mkuu wa Dola akiwasilishwa na Gavana Mkuu. Mamlaka iko mkononii wa waziri mkuu na serikali yake.

Serikali[hariri | hariri chanzo]

Muundo wa utawala ni ya shirikisho. Kuina majimbo 6 ya kujitawala pamoja na maeneo ambayo ni moja kwa moja chini ya serikali ya shirikisho.

Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Australia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Nchi_na maeneo ya Australia na Pasifiki
Australia | Fiji | Guam | Hawaii | Kaledonia Mpya | Kiribati | Kisiwa cha Pasaka | Mikronesia | Nauru | New Zealand | Niue | Pitcairn | Polynesia ya Kifaransa | Palau | Papua New Guinea | Samoa | Samoa ya Marekani | Visiwa vya Cook | Visiwa vya Mariana ya Kaskazini | Visiwa vya Marshall | Visiwa vya Solomon | Tonga | Tuvalu | Vanuatu | Wallis na Futuna