Wallis na Futuna

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Wallis na Futuna baharini.

Wallis na Futuna ni eneo la ng'ambo la Ufaransa katika Bahari ya Pasifiki kati ya Fiji na Samoa.

Eneo lake ni visiwa vitatu vyenye jumla ya kilomita za mraba 274.

Idadi ya wakazi ni 13,000. Kwa upande mmoja kuna kisiwa cha Wallis na kwa upande mwingine visiwa vya Futuna. Umbali kati yake ni takriban kilomita 200.

Wakazi walio wengi ni Wapolynesia wakiongea lugha za Kipolynesia pamoja na Kifaransa.

Wakazi walio wengi huishi kwa kilimo cha kujikimu. Uchumi hutegemea misaada kutoka Ufaransa. Katika miaka iliyopita utalii umeanza kuchangia katika pato.

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.