Kifaransa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Matumizi ya Kifaransa duniani: Buluu nyeusi: Lugha ya kwanza ya watu wengi; buluu: Lugha rasmi;
Buluu nyeupe: Lugha ya mawasiliano; Kijani: Lugha ya watu wachache

Kifaransa (kwa Kifaransa: français) ni lugha ya Ufaransa (pamoja na maeneo yake ya ng'ambo), Ubelgiji ya Kusini, Uswisi ya Magharibi, Luxemburg na Kanada. Inazungumzwa pia katika nchi nyingi za Afrika kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Senegal, Mali, Shelisheli, Chad, n.k., Asia ya Kusini na Amerika zilizokuwa makoloni ya Ufaransa.

Wasemaji[hariri | hariri chanzo]

Takwimu kuhusu matumizi ya Kifaransa hutofautiana. Kadirio ndogo lasema kuna watu milioni 87 wanaotumia Kifaransa kama lugha ya kwanza, na tena milioni 100 wanaoitumia kama lugha ya pili. Kadirio kubwa lataja milioni 112,6 wasemaji wa lugha ya kwanza pamoja na milioni 60,6 wenye uwezo wa kutumia Kifaransa karibu kama lugha ya Mama. Halafu hutajwa takriban milioni 100 -110 wanaotumia Kifaransa kikazi, kibiashara au masomoni jumla takriban milioni 300 wasemaji wa Kifaransa duniani.

Historia ya lugha[hariri | hariri chanzo]

Kifaransa ni kati ya lugha za Kirumi. Asili yake ni Kilatini lugha ya Waroma wa Kale. Hadi mwaka 50 KK watu waliokalia Gallia (eneo la Ufaransa wa leo) walitumia lugha mbalimbali za Kikelti. Baada ya uvamizi na Waroma Gallia ilikuwa sehemu ya Dola la Roma. Lugha ya Kilatini ilienea hadi kuwa lugha ya watu wengi. Kikelti kimebaki hadi leo katika maeneo madogo kama Ubritani.

Kilatini hiki jinsi kilivyojadiliwa na watu wa kawaida katika Gallia kilipokea kiasi cha maneno na matamshi na lugha ya Kikelti. Baada ya mwisho wa Dola la Roma lugha iliendelea kubadilika haraka zaidi. Makabila ya Kigermanik walivamia Gallia na kuleta athira ya lugha zao.

Haya yote yaliunda lugha ya Kifaransa ambayo ni lugha karibu sana na Kilatini hivyo pia na lugha kama Kiitalia, Kihispania na Kireno.

Kifaransa kilichokuwa rasmi kilifuata lahaja ya eneo la Paris. Tangu 1634 kuna Akademia ya Kifaransa aabayo ni taasisi ya kulinda usafi wa lugha.

Kifaransa kilienea kimataifa kwa sababu Ufaransa ilikuwa taifa lenye maendeleo mengi katika Ualya. Kifaransa kilikuwa katika nchi nyingi lugha ya elimu na pia ya mawasiliano ya kimataifa jinsi ilivyo siku hizi Kiiingereza mahali pengi.

Baada ya Ufaransa kuwa nchi yenye koloni lugha ilisambazwa hata nje ya Ulaya. Ubelgiji yenye Kifaransa kama lugha rasmi ilikuwa pia na koloni na kupeleka lugha huko.

Hali ya Lugha kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Kifaransa ni lugha ya kitaifa, lugha rasmi, lugha ya utawala au lugha ya mawasiliano katika nchi zifuatazo:

Ulaya[hariri | hariri chanzo]

  • Lugha ya kitaifa pamoja na lugha nyingine
Uswisi (lugha rasmi hasa katika mikoa ya magharibi)
Ubelgiji (lugha rasmi hasa katika jimbo la Wallonia)
Luxemburg
  • Lugha rasmi kimkoa
Italia katika mkoa wa Val d'Aoste

Afrika[hariri | hariri chanzo]

Lugha rasmi ya nchi zifuatazo

  • Lugha ya utawala:
Mauritania
Djibouti
  • Lugha ya elimu na mawasiliano, lakini wala lugha ya kitaifa wala lugha rasmi katika
Algeria
Moroko
Tunisia.

Asia[hariri | hariri chanzo]

Amerika[hariri | hariri chanzo]

  • Lugha rasmi ya Haiti
  • Lugha ya utawala katika Jamhuri ya Dominika
  • Moja ya lugha mbili za kitaifa katika Kanada; ni lugha rasmi ya pekee katika jimbo la Quebec (13% ya Wakanada wote hujua Kifaransa pekee, 18% wanajua lugha zote mbili)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]